Habari za Teknolojia

Faida ya Facebook inazidi kupanda, Sasa ina watumiaji zaidi ya Bilioni 2

Kulingana na ripoti ya matokeo ya mtandao huo faida ya mtandao wa facebook imepanda katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huku mtandao huo ukikaribia kupata wateja bilioni 2.

Mtandao wa kijamii wa Facebook unakadiriwa kuwa na wateja bilioni 2 duniani kote.

Kila mwezi idadi ya watu wanaotumia mtandao huo iliongezeka hadi bilioni 1.94, ambao watu bilioni 1.3 huutumia kila siku. Kampuni hiyo ya Kiteknolojia liyo na makao makuu yake nchini Marekani iliripoti faida za takriban dola bilioni 3 katika robo ya kwanza ya mwaka ambayo ni ongezeko la asilimia 76 kwa mwaka.

Siku ya Jumatano ,Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg alitangaza kwamba atawaajiri watu 3000 zaidi kuweka maudhui ya wastani katika mtandao huo. Akizungumza baada ya ripoti hiyo ya matokeo ,bwana Zuckerberg alisema kwamba idadi ya watumiaji wake wameipatia Facebook fursa ya kupanua jukumu la mtandao huo ,kuanzisha runinga, afya na siasa.

SOMA NA HII:  Snapchat imeondoa Channel ya Al Jazeera nchini Saudi Arabia

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.