Fahamu Faida & Hasara za Kutumia Kompyuta ya Windows 8


Uchambuzi wangu kuhusu kompyuta ya Windows 8 unakupa ufahamu kamili kuhusu faida na hasara za Windows 8. Katika makala hii, nitakupa uzoefu wangu wakati wa kutumia Windows 8.

kompyuta
Kwa mtazamo wangu, ni mfumo bora wa uendeshaji. Tunajua kila kitu kina faida na hasara. Katika makala hii, nitaelezea sifa na udhaifu wa mfumo wa uendeshaji wa Windows 8.

Faida za Kutumia Windows 8 PC

  • Muonekano wake ni tofauti kabisa na matoleo ya awali ya Windows. Utaona utofauti. Inatoa vifungo (thumbnails) vya programu zote kwenye skrini ya mwanzo (start screen). Ikiwa hutaki kutumia skrini ya kuanzia , unaweza kwenda kwenye eneo la kawaida.
  • Utafutaji ni rahisi sana. Ni chombo chenye ufanisi sana katika Windows 8.Unaweza kutafuta faili, programu, na mipangilio. Kwa mfano: – Fanya unataka ku-unistall programu. Katika matoleo ya awali unapaswa kwenda kwenye control panel kisha programs baada ya hapo, utaweza ku-uninstall programu unayotaka . Katika Windows 8 unakwenda kwenye start screen na kisha unaandika uninstall the program. Usiulize unaandika sehemu gani. Bila shaka, hakuna mahali maalum kwajiri ya kuandika; unatakiwa kutumia keyboard keys. Windows itatafuta moja kwa moja, na unaweza kuingia moja kwa moja katika eneo la ku-Uninstall programu. Pia kama unataka kubadilisha mipangilio yoyote ile, unaandika tu katika skrini ya mwanzo kama katika utafutaji wa Google, itakupa programu maalum.
  •  Utajisikia raha kuhama kutoka kwenye programu moja hadi programu nyingine. Muonekano (Visual appearance) ni mzuri sana katika Windows 8.
  • Multi-tasking ni laini sana. Unaweza kutumia programu mbili kwa wakati mmoja kwenye desktop. Naweza kusema sio windows mbili, ila ni programu mbili. Katika Windows 8 kila kitu ni programu. Hata desktop ni programu.

Hasara za Kutumia Windows 8 PC

  • Inafanya kazi taratibu.
  •  Inatumia RAM kubwa. Hata wakati wa mwanzo, inatumia zaidi ya RAM 1 GB. Ili kutumia Windows 8 kwa ufanisi, lazima uwe na RAM 4 GB. Tunaweza kutumia kwa RAM 2 GB, lakini unapoendesha programu yoyote, itakuwa inagandaganda.
  •  Ina IE10 ambayo ni bora kwa kimuonekana lakini inafanya kazi polepole. Unapotumia Internet Explorer katika Windows 8, inachukua zaidi ya RAM MB 250. Inashauriwa kutumia Google Chrome au vivinjari vinginevyo.
  • Hutaona chaguo la shutdown kwenye desktop. Bila shaka, unaweza kutatua tatizo hili kwa kuunda njia ya mkato ya kuzima kompyuta (shutdown shortcut) kwenye desktop. Unaweza pia kutatua suala hili kwa ku-update Windows 8 kuwa Windows 8.1.
  • Hakuna start icon kwenye desktop, pia hutatuliwa kwa ku-update kwenye Windows 8.1. Windows 8.1 ni sasisho la bure linalotolewa na Microsoft.
  • Desktop widgets hazipo. Unatakiwa ku-install programu ya widget. Kwa kuweka desktop widgets kasi ya windows 8 itapungua zaidi.

 Hitimisho

Ikiwa unataka kupata uzoefu mpya wamuonekano, tumia Windows 8. Ikiwa unataka kasi ya juu,usitumie mfumo huu wa uendeshaji endelea kutumia Windows 7. Unataka kununua Windows 8, napendekeza kufanya ununuzi wako kwenye Microsoft store tu

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA