Home Nyingine Faida 7 za kumkumbatia Mpenzi Wako

Faida 7 za kumkumbatia Mpenzi Wako

0
0

Naandika makala hii maalumu kwajiri ya wapenzi, sio kwajili ya watoto wadogo. Hata hivyo ngoja niulize..

Unajua ngozi yako ndio kiungo kikubwa zaidi kwenye mwili wako?

…Ndio ni kweli na unapaswa kuitumia kuifaidisha ndoa yako. Kutumia muda wako kumkumbatia mpenzi wako kabla na baada ya kukutana kimwili inaweza kuleta maajabu kwenye mahusiano yenu.

Ngozi yako inapokuwa kwenye mawasiliano na ngozi ya mpenzi wako  mnaungana kihisia katika kiwango kikubwa zaidi. Kwa hiyo leo nashare nawe faidi za kukumbatiana na mpenzi wako.

1. INABORESHA MAWASILIANO 

Kuwasiliana bila ya kutumia maneno inachukua asilimia 93% ya jinsi wewe na mpenzi wako mnavyoingiliana. Kwa kukumbatiana kimahaba kunakuwa na majadiliano bila maneno.

2. HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA:

Unapomkumbatia mkeo husaidia kuzalisha kichocheo (homoni) cha furaha kiitwacho oxytocin. Homoni hii hufanya kazi ya kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Hilo pia hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa na maumivu ya kichwa na maradhi mengine.

3. USINGIZI MARIDHAWA:

Wanandoa wanapokumbatiana husaidia kulala vizuri. Tafiti mpya zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza cortisol na hivyo kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Pindi cortisol inapopungua mwilini, moja kwa moja usingizi huwa mzuri na mwanana.

4. Unapomkumbatia inaweza kusababisha raha

Hasa mambo yanapofikia kwenye hatua ya kucheza, lakini kabla ya hapo furahia ladha ya mgusano wa ngozi zenu kabla ya kusonga mbele… Moyo wako unatakiwa kuuhudhurisha katika eneo na muda wa mgusano huo ili kujenga uaminifu na hisia za ushirika.

5. Kukumbatiana huwapa fursa ya kuwasiliana bila kuongea.

Na hili ni jambo maridhawa kabisa kwa wanandoa kuzidi kuwa karibu.

6. NI DAWA YA FADHAA:

Kimbilia kitandani. Kumbuka kuwa kitanda kipo kwa ajili hiyo. Achana na kitabu, televisheni, simu, tablet na mambo mengine kama hayo. Kumbatio litakusaidia kumakinika na kupata utulivu.

7. HUWAPA HISIA ZA KURIDHIANA NA KUTOSHEKA:

Mnapokumbatiana bila kuwa na lengo la kuingia kwenye tendo la ndoa, mtapata hisia kubwa ya kuridhika na ndoa yenu. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa wanandoa wanaokumbatiana wanaridhika sana na ndoa zao kuliko wale wasiokumbatiana

Nafikiri sasa utakuwa umejifunnza kitu kutoka kwenye maneno machache niliyoshare nawe.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *