Fahamu Ukweli Kuhusu KeyBoards


Hapa kuna ukweli wa kuvutia kuhusu Kibodi (kutoka Kiingereza: “keyboard”), si tu keyboard maarufu ya QWERTY, bali tunaangalia na baadhi ya aina nyingine za keyboards zinazopatikana. Angalia ukweli huu!

Kwenye keyboard ya kawaida ya QWERTY, neno ‘Typewriter’; ni neno refu sana linaloweza kuandikwa kwa kutumia herufi zilizo kwenye safu moja tu ya keyboard, ni kweli, herufi za kwenye mstari wa juu tu.

QWERTY Keyboard
QWERTY Keyboards

QWERTY Keyboard iliundwa na Christopher Sholes mwaka wa 1868 na sasa ni aina ya keyboard inayotumiwa na watu wengi zaidi duniani. Pia inajulikana kama Universal keyboard. Tukirudi nyuma mwaka 1868 walikuwa na mashine za uchapishaji maarufu kama “typewriters” na kutengeneza kibodi katika mfumo huu ilikuwa njia ya kuzuia mashine hiyo kufanya kazi vibaya. Typewriter ya kwanza ilikuwa inachapa herufi kubwa tu . QWERTY keyboard kwenye kompyuta za kawaida bado inatumika zaidi kwa sababu ya gharama nafuu na ni rahisi kutumia.

Dvorak keyboard
Dvorak keyboard

Mwaka 1932 Profesa August Dvorak alijaribu kutengeneza keyboard nyingine ambayo itakuwa rahisi kutumia kuliko QWERTY. Lengo la Dvorak kutengeneza kibodi iliyo bora zaidi kuliko ya kwanza ilikuwa kwa kupanga herufi kulingana na mzunguko. Kibodi ilikuwa na herufi tamfu zote tano na konsonanti tano za kawaida kwenye safu ya kati ambazo ni: AOEUIDHTNS. Herufi kwenye safu ya kati, pia inajulikana kama “home row”, inafanya jumla ya 70% ya kazi. Katika QWERTY zinafanya kazi 32% tu. Herufi zisizo tumika mara kwa mara zilikuwa kwenye safu ya chini, kwa sababu ni safu ngumu zaidi kufikia.

keyboards maalumu kwajili ya gaming

Pia kuna keyboards maalumu za michezo ya kubahatisha (gaming keyboards) ambazo hupangwa kwa njia ambayo herufi zinazotumika zaidi wakati wa kucheza games hujumuishwa sehemu moja ili iwe rahisi kutumia. . Gaming keyboards zinatoa mwaga pia, ili keys zionekane kwa urahisi. Keyboards za awali hazikutengenezwa hasa kwa madhumuni ya gaming, kwa maoni yangu, hili ni wazo zuri sana.

SOMA NA HII:  Jinsi Ya Kufuta Akaunti Yako Ya Facebook Moja Kwa Moja!

Hakika natumaini wewe si mtaalam wa keyboard na umejifunza kitu kipya katika chapisho hili. Je, kuna mtu yeyote anaye kutumia keyboard ya Dvorak ? Ikiwa unatumia, toa maoni tafadhali.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA