Fahamu Mfumo wa Uendeshaji Unaotumika Zaidi #Android


Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa asilimia 50 ya simu za android zinatumia mfumo wa Android 6.0, 7.0, na 7.1.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Android zilizotolewa na Google, mfumo wa uendeshaji wa Android 6.0 Marshmallow una hisa 26%, na 7.0 na 7.1 zina 23% na 7.8% kwa mtiririko huo.

Android 8.0 na 8.1 – kwa jina jingine Android Oreo, na toleo la hivi karibuni la mfumo wa uendeshaji – zipo kwa  4.1% na 0.5% kwa mtiririko huo.

Matoleo mengine ya OS ambayo yana sehemu kubwa ni pamoja na Android 5.1 kwa asilimia 18% na Android 4.4 kwa 10.5%.

Sababu ya sehemu kubwa ya mifumo ya uendeshaji ya zamani kutawala soko ni kwamba watengenezaji wa simu za mkononi au mitandao ya simu imeshindwa kushinikiza sasisho za OS kwa baadhi ya simu za mkononi za Android.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA