Fahamu mahitaji na namna ya Kupata Mashine ya Risiti ya Kielektroniki (EFD)


Kwa kifupi kabisa EFD ni mashine zilizotengenezwa kwa ajili ya kutumika katika biashara kwa ajili ya kudhibiti mauzo na mfumo wa mali unaofuata masharti yaliyoelezwa na sheria.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato mwaka 2012, mtoa huduma hapa Tanzania anapaswa kuwa na mashine ya risiti za kielekroniki (EFD) kuhalalisha mauzo anayofanya.

Mashine hizi huunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na kuwasilisha taarifa muhimu ambazo husaidia katika ukadiliaji wa kodi. Lakini kabla ya kuendelea ni vizuri ujue kuwa Mashine hizi haziwahusu wafanyabiashara wa sekta isiyo rasmi kama vile mama ntilie na wamachinga kwa sababu hawana sehemu maalum ya kufanyia biashara.

Kupata mashine za risiti za kielektroniki ni rahisi sana unahitaji kuwa na mambo machache sana ili uweze kuwezesha kupata mashine hiyo.

SOMA NA HII:  Netflix sasa ina wanachama milioni 125

Mahitaji ili kupata EFD ni Haya:

  • ¬†Kiasi cha Fedha cha kununua Mashine hiyo (Angalia Wakala Hapa)
  • Nakala ya namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) (Unaweza Kupata Hapa)
  • Namba ya usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

Kwa kampuni Unahitaji vyote hivyo hapo juu pamoja na :

Na hayo ndio maelezo mafupi jinsi ya kupata mashine hiyo ya EFD au Electronic Fiscal Devices, kama unataka maelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti ya TRA au piga simu za bure kwa Tanzania 0800 750 075  au 0800 780 078.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *