KompyutaMaujanjaMicrosoft

Fahamu Jinsi Ya Kurudisha Kazi Iliyopotea Katika Ms Office

Umewahi kukutwa na tatizo la kukatika kwa umeme wakati unaandika vitu muhimu kwenye Kompyuta yako na ukashindwa kujua nini cha kufanya kwa sababu bado ulikuwa haujahifadhi (save) kazi yako?

Ondoa shaka leo nitakuelekeza jinsi ya kurudisha kazi yako uliyoifunga kwa bahati mbaya au kwa sababu ya kukatika kwa umeme katika Microsoft Word, Microsoft Publisher, Microsoft Excell pamoja na Microsoft Power Point.

Njia hii inafanya kazi vizuri zaidi kwa vifurushi (packages) za Microsoft Office 2010,2013 na 2016 kwa sababu kazi unayoichapa huwa inahifadhiwa kwenye draft bila ya wewe kujua. Unaweza ukaset muda wa kazi kuwa saved automatically katika Tab ya save, ila kwa kawaida huwa inakuwa ni dakika 10.

Njia za kufuata ili kurudisha kazi yako uliyoifunga kwa bahati mbaya katika moja ya bidhaa za Ms Office

  • Fungua Microsoft Office uliyokuwa ukitumia kama ni Word, Excel, Publisher au Power point
  • Bonyeza File Tab, upande wa kushoto juu kabisa, kisha bonyeza Recent
  • Bonyeza Recover Unsaved Document kama upo kwenye Ms Word, na Recover Unsaved Workbook kama upo kwenye Excel na Recover Unsaved Presentation kama upo kwenye power point.
  • Kazi yako iliyohifadhiwa kwenye draft itaonekana na utaifungua ili kuendelea kuiedit (kuifanyia kazi)
  • Baada ya kuifungua sasa kumbuka kuisave ili kupunguza uwezekano wa kuipoteza tena pale umeme unapokatika.
SOMA NA HII:  Orodha ya njia za mkato za keyboard katika Mozilla Firefox

Sasa utakuwa umefahamu jinsi ya kurudisha kazi yako iliyopotea kwa bahati mbaya, na kama ulikuwa unaandika makala au unachapa kazi ndefu nadhani una kila sababu yakufurahia.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment, je umekutana na tatizo lolote katika kurudisha kazi zako?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku, Karibu Kwa Pamoja Tujenge Jamii Ya Wanateknolojia!.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako