Fahamu Huduma za Timu ya Mwitikio wa Kukabili Majanga ya Kompyuta Tanzania


Timu ya Mwitikio wa Kukabili Majanga ya Kompyuta Tanzania, kwa kifupi TZ-CERT,  ni timu yenye jukumu la kuratibu mwitikio wa  matukio ya usalama wa mtandao  ngazi ya taifana kushirikiana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa  vinavyojishughulisha na usimamizi wa matukio ya kiusalama wa  mtandao.   TZ-CERT ilianzishwa chini ya Kifungu 124 cha Sheria ya Elektroni na Posta (EPOCA) Na. 3 ya 2010 ndani ya mfumo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kwa sasa TZ-CERT inatoa huduma zifuatazo kwa washirika na umma kwa jumla.

(i) Tahadhari na Onyo

Kutokana na kukua kwa matishio ya usalama mtandaoni, TZ_ZERT wakati wote inafuatilia matishio ya kiusalama ya mtandao na uwezekano wa kudhuriwa na kuweza kushauri washirika na umma kwa jumla.

(ii) Mwitikio wa Tukio

Kwa utaalam wa usalama wa mtandao, TZ-CERT yaweza sasa kufanya kazi na asasi za washirika kuitikia kwa matukio yote ya kiusalama ya mtandao katika mitandao yao mahususi. Pamoja na hayo TZ-CERT inatoa msaada wa hatua kwa hatua  kwa asasi inayokabiliwa na mashambulio ya kiusalama.

(iii) Mwamko wa Usalama wa Mtandao

Ikiwa na jukumu la kuboresha usalama wa mtandao nchini, TZ-CERT inafanya kazi ya kusambaza taarifa za kiusalama wa mtandao kwa jamii. Hii inajumuisha kuendeleza utendaji wa mfano kwa watumiaji wa teknolojia.

TZ-CERT itaboresha  huduma zake  na kulenga utoaji wa huduma nyingine za  mtandao kwa jamii  ikiwemo Ukaguzi  wa usalama na tathmini, Uchambuzi wa mifumo tumizi haribifu,Ugunduzi wa kuingiliwa, Uchambuzi wa hatari na Ushauri wa Usalama.

Kwa Taarifa Zaidi Tembelea Tovuti ya TZ-CERT

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA