Facebook imeanzisha Watch, kichupo (tab) kipya kwenye mtandao huo wa kijamii ambacho huonyesha maonyesho (shows) mbalimbali kwa watumiaji kwa urahisi.

Facebook-mediahuruWatch itakuwa inapatikana kwenye simu, kwenye desktop na laptop, na katika app ya TV, ikiwa na orodha ya ufuatiliaji ambayo inakuwezesha kuangalia vipindi baadaye.

Ingawa, baadhi ya maonyesho yatakayo onyeshwa na Watch yamefadhiliwa na Facebook, watengenezaji wa kujitegemea wanaweza pia kujiandikisha kwenye jukwaa ili kupata Ukurasa wa Kuonyesha (sawa na Kurasa za bidhaa), ambao mashabiki wanaweza ku-follow na kupata hizo video.

Watch imetengenezwa ili kukusaidia kugundua maonyesho mapya, yaliyoandaliwa karibu na vitu ambavyo marafiki zako na jumuiya wanaviangalia. Kwa mfano, utakutana na vipengele kama “Most Talked About,” ambacho kinaonyesha vitu vilivyo zungumziwa zaidi, “What’s Making People Laugh,” ambacho kinajumuisha shows ambazo watu wengi wametumia reaction ya “Haha”, na “What Friends Are Watching,” ambayo husaidia kukuungana na marafiki kuhusu shows ambazo na wao wanafuata.

SOMA NA HII:  Fahamu Maana ya Mtandao wa Intaneti na Faida Zake

Ujio wa Watch, unafanya wabunifu na waandishi waweza kupata watazamaji, kujenga jumuiya ya mashabiki wenye shauku, na kupata pesa kwa kazi yao. Facebook pia ina mpango wa kuanzisha “ad breaks” katika shows ili kuzalisha mapato kwenye Watch.

Vipengele vyote hivi, vinaenda pamoja na msingi wake wa watumiaji wa watu bilioni mbili ulimwenguni pote, Facebook inaweza kuwa mshindani mkubwa wa Youtube na kwa huduma hii mpya.

Huduma mpya itaanza kutumiwa na kundi dogo la watu nchini Marekani kabla ya kuanza kutumika duniani kote.

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako