Intaneti

Facebook kuzindua huduma ya usajili wa habari kufuatia malalamiko kutoka kwa vyombo vya habari

on

Facebook imetangaza mipango ya kuanzisha huduma ya “news subscription” kwenye mtandao huo wa kijamii unaoongoza kuwa na watumiaji wengi duniani. Kipengele hicho kitatengenezwa juu ya huduma ya “Facebook Instant Articles”, ambayo inaruhusu waandishi wa habari kusajili stori zao ili zisomwe kwa haraka bila ya kutoka kwenye Facebook.

Kwa mujibu wa mkuu wa ushirikiano wa habari wa Facebook, Campbell Brown, mpango huo ni kuruhusu wasomaji kupata habari/makala 10 bure, na makala zinazofuata zikiwa zimefungiwa kwenye paywall kutoka kwa mchapishaji. Msomaji ataelekezwa kwenye tovuti ya mchapishaji kujiandikisha kwajili ya usajili.

Facebook imesema itaanza kujaribu huduma hiyo mwezi Oktoba, na mambo yote yakienda vizuri, kipengele hicho kitatumiwa na watu wote kuanzia mwaka 2018.

SOMA NA HII:  Ripoti : Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23

“Moja ya mambo tuliyoyasikia katika mikutano yetu na magazeti na waandishi wa kidigitali ni kwamba ‘tunataka bidhaa ya usajili – tunataka kuona malipo katika Facebook,'” Brown alisema katika Mkutano wa Innovation Digital Publishing jijini New York City Julai 18. “Na hicho ni kitu tunachofanya sasa. Tunaanzisha huduma ya kujisajili. ”

Taarifa hii imekuja kufuatia wito wa “U.S. Congress” kutoka kwa vyombo vya habari zaidi ya 2,000 wiki iliyopita kujadiliana na Google na Facebook. Mashirika hayo yalisema kuwa Google na Facebook zina ushawishi mkubwa jinsi habari “zinavyoonyeshwa, zinavyopewa kipaumbele, na zinavyoingiza mapato” mtandaoni na zinapata faida kubwa kutoka na mauzo ya matangazo ya digitali. Mpaka sasa.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

2 Comments

 1. Kulwa

  September 30, 2017 at 7:48 am

  Mimi Niko Tanzania Nahitaji bidha

  • Mediahuru

   September 30, 2017 at 8:51 am

   karibu ndugu Kulwa kwenye tovuti ya mediahuru. Samahani unaweza kueleza vizuri unahitaji bidhaa gani?

Leave a Reply

Your email address will not be published.