Facebook kuonyesha michezo ya NFL duniani nzima


Facebook na “National Football League” wametangaza mipango ya kuonyesha video highlights za michezo ya NFL kwa watumiaji wa mtandao wa kijamii unaoongoza duniani kote.

“NFL Game Recaps” na mambo muhimu kutoka kwenye michezo 256 ya kawaida ya msimu pamoja na playoffs na Super Bowl zitapatikana kwa watumiaji duniani kote kwenye Facebook, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa NFL Media, sehemu ya ligi hiyo inajihusisha na masuala ya tehama ya ligi, itatoa maudhui kutoka kwenye Filamu za NFL kwenye jukwaa la Facebook Watch .

Mpango huo ni wa hivi karibuni kuleta maudhui ya michezo kwenye majukwa ya mtandao kama vile Facebook, Twitter na Amazon.

“Tuna mamilioni ya mashabiki kwenye Facebook, na wanaendelea kuonyesha hamu ya ajabu ya maudhui ya NFL,” alisema Hans Schroeder, afisa wa uendeshaji wa NFL Media.

“Tunategemea kuleta seti ya highlights na maonyesho (shows) kutoka NFL na klabu zetu kwa mashabiki wetu kwenye Facebook.”

Dan Reed, mkuu wa ushirikiano wa michezo ya kimataifa wa Facebook, alisema mpango huo “utatoa chanjo kamili wakati wa kuwezesha jumuiya ya mashabiki wa NFL kwenye Facebook ili kutazama na kuzungumzia stori zinazotokea kila wiki.”

NFL mapema mwaka huu ilitoa haki za kusambaza michezo ya Alhamisi usiku kwa Amazon, baada ya mpango sawa na Twitter mwaka jana. Verizon, wakati huo huo, ilishinda haki za kusambaza mchezo wa NFL wa Septemba 24 uliofanyika London.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA