Facebook kuonyesha magari yanayouzwa na wafanyabiashara wa magari (FB)


Facebook inaongeza orodha ya magari (car listings) kutoka kwa wafanyabiashara wa magari kwenye tab yake ya Marketplace. Hii ni hatua nyingine kubwa ya kutaka kuingia kwenye biashara ya mtandaoni (e-commerce).

  • Facebook inaongeza orodha za magari yanayouzwa kutoka kwa wafanyabiashara wa magari kwenye tab yake ya Marketplace.
  • Lakini mtandao huu wa kijamii haujaruhusu watu kufanya malipo ndani ya jukwaa lake – bado.

Facebook imeongeza kwa kasi idadi ya magari ambayo inaweza kusaidia kuuza kwa kushirikiana na Edmunds, Cars.com, na wengine.

SOMA NA HII:  Je natakiwa kumiliki website au blog ?

Washirika wapya watasaidia kuipa umaarufu sehemu ya soko ya Facebook kwa magari kuuzwa na wafanyabiashara wa magari badala ya orodha ya kuuzwa-na-mmiliki ambayo inapatikana sasa. Hatua hiyo inaendeleza nia ya Facebook kuwa e-commerce, ingawa mtandao huu wa kijamii bado hauruhusu shughuli za kifedha zifanyike kwenye Marketplace yake.

Badala yake, wale wanaovutiwa na magari yaliyowekwa na wafanyabiashara kwenye Marketplace wataweza kuwasiliana na muuzaji moja kwa moja kupitia Facebook Messenger. Facebook pia itawawezesha watumiaji kulinganisha bei ya magari yaliyoorodheshwa.

Facebook imeshirikiana na idadi kubwa ya washirika wa nje, kama eBay kwa dili zake za kila siku na Eventbrite kwa ajili ya kuuza tiketi za matukio mbalimbali, lakini bado hairuhusu “transactions” zifanyike kwenye jukwaa lake.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA