Facebook imesai deal kubwa na Universal Music


Facebook Inc imesaini mkataba ambao utaruhusu mtandao huo wa kijamii kutumia nyimbo na wasanii kutoka lebo kubwa ya kurekodi muziki dunia, Universal Music Group, kwenye majukwaa yake.

Mpango huo ulitangazwa siku ya Alhamisi kutatua mgogoro wa muda mrefu, Facebook imekubali kulipa fidia kwa kampuni hiyo na wasanii ikiwa ni pamoja na Taylor Swift pale watumiaji wanapoweka video ambazo zinajumuisha kazi zenye hakimiliki. Mkataba huo unajumuisha Facebook, Instagram na Oculus,Universal imesema kampuni hiyo itakuwa “mchango mkubwa” kwenye sekta ya  muziki.

Deal hilo linafanya Facebook kuwa mpinzani wa moja kwa moja wa YouTube ya Google, ambayo ni sehemu maarufu zaidi kwenye mtandao kwajili ya kusikiliza muziki.

SOMA NA HII:  Mitandao ya kijamii kutumika kwenye kuomba visa Marekani

Kufanya kazi na Facebook kunaleta shinikizo kwa YouTube, ambayo imekuwa jukwaa lenye nguvu katika sekta ya muziki kama chombo cha masoko na njia ya kutambulisha wasanii wapya. Tovuti hiyo ya video inayomilikiwa na Google mwezi huu iliweka saini mkataba mpya wa muda mrefu na Universal Music, inayomilikiwa na Vivendi SA, na Sony Music Entertainment.

Dunia ya mtandaoni imekuwa chanzo cha ukuaji kwa sekta ya muziki, na huduma kama Spotify na Apple Music kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi zimekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wake.

Facebook mwezi Januari ilimwajiri Tamara Hrivnak, mtendaji wa zamani wa sekta ya muziki ambaye amewahi kufanya kazi Google na YouTube, ili kuongoza juhudi zake za maendeleo ya muziki.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA