Facebook Imefikishwa Mahakamani kwa Kosa la Kufatilia Simu & Sms za Watumiaji


Baada ya habari kuvunja kwamba apps za Facebook Messenger na Lite zinafatilia simu unazopiga na ujumbe mfupi unaotuma kwenye vifaa vya Android, mtandao huo wa kijamii ulitoa taarifa kwamba haukufanya hivyo kwa siri.

Ilipata ruhusa ya kufikia data hizo kutokana na mfumo wa ruhusa wa Android, na imekuwa inakusanya taarifa kwa watumiaji ambao walikubali kutoa ruhusa kwa app kufatilia mawasiliano yao.

Maelezo hayo, hata hivyo, hayakutosha kwa watumiaji watatu ambao wamefungua mashitaka dhidi ya mtandao wa kijamii wa facebook, kwa kosa la kukiuka faragha yao kwa kukusanya simu zao na ujumbe mfupi.

Kwa mujibu wa Reuters, kesi imefunguliwa katika mahakama ya eneo la kaskazini mwa jiji la California nchini Marekani na wanatafuta nguvu zaidi kusimama kwa niaba ya watumiaji wote walioathiriwa na mtandao huo.

Bila shaka, hakimu bado anaweza kuamua kama watu wa kutosha waliathiriwa na suala hilo kabla ya kesi kuendelea kwa hatua zaidi za kisheria.

Katika ufafanuzi wa Facebook, imesema haikuuza data zote za simu na ujumbe mfupi kutoka kwenye simu za Android na kwamba haikuwa na uwezo wa kuona sms za watu.

Bado inasubiriwa kuona kama kampuni ina uhakika wa kutosha kwa watu wengi au watumiaji wa kutosha watakuja kuunga mkono kesi hiyo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA