Nyingine

Europa League!! Anderlecht 1-1 Man United (MATOKEO)

Manchester United wameshindwa kuondoka na ushindi ugenini dhidi ya Anderlecht baada ya kulazimishwa suluhu ya 1-1 katika hatua ya robo fainali.

Henrikh Mkhitaryan alianza kuiandikia bao United baada ya kazi nzuri ya Marcus Rashford Hii ikiwa ni dakika ya 37. Mkhitaryan amefunga katika michuano minne mfululizo ya United ya ugenini

Kipindi cha kwanza Manchester United ikaenda mapumzikoni ikiwa kifua mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikishambulia lango la mwenzake.

United ikiamini imemaliza kazi dakika ya 87 Leander Dendoncker akaiandikia Anderlecht goli la kusawazisha na kuhitimisha mchezo huo.

Marudio ya mchezo huu ni wiki ijayo na zamu hii United itakuwa nyumbani Old Trafford.

SOMA NA HII:  Kwa nini Mwanamke Anaweza Kuweka Picha Zake Za Uchi Kwenye Simu Yake? - Uzoefu Binafsi

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.