Habari za TeknolojiaIntaneti

Ethiopia yazima mtandao wa Intaneti kupambana na kuvuja kwa mtihani

Linapokuja suala la udanganyifu, mamlaka za shule siku zote zina hakikisha kuwa wanakuwa na nguvu kubwa kuzuia vitendo vichafu wakati wa mitihani – mfano kuangalia kama mwanafunzi ameandika majibu kwenye sehemu zake za mwili / Math set/ calculator / four figure table huku wengine wakikusanya simu za wanafunzi- lakini kuna nchi imetumia mbinu iliyovuka mipaka kwa kuzima kabisa intaneti nchi nzima kwa lengo la kuwazuia wanafunzi kufanya udanganyifu.

Jumanne, wakati wanafunzi wa Ethiopia  (wanafunzi wa darasa la 10 milioni 1.2 na wanafunzi wa daraja 12 zaidi ya 300,000) walikuwa wanajiandaa kufanya mitihani siku ya Jumatano, mtandao wa nchi hiyo ulifungwa ili kuzuia uvujaji wa mitihani.

Jambo hili halijashangaza wengi nchini humu kwa sababu huu ni mwaka wa pili tukio kama hilo linatokea .

Sasa, kitu kinachoshangaza ni ukweli kwamba kuzima mtandao wa intaneti kunaweza kusiwe na tofauti kubwa linapokuja suala la kuvuja kwa mtihani kwa sababu Ethiopia ni moja ya nchi zenye viwango vya chini kabisa katika matumizi ya mtandao na kuunganishwa kwa njia ya simu za mkononi (Quartz), ukweli ni kwamba, asilimia 4 ya wakazi wa Ethiopia ndio wanatumia huduma ya mtandao.

SOMA NA HII:  Ifahamu treni yenye spidi kali zaidi duniani

Kwa hiyo, Ethiopia:

Kama ukiniuliza mimi, Sidhani kama intaneti inaongeza kasi ya kuvuja kwa mitihani, kwa sababu naamini mitihani inavuja huko huko inakotengenezwa.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako