Android

“Error” kwenye simu ya HTC 10 imesababisha matangazo kuonekana kwenye keyboard app

on

HTC 10 bado inaendelea kufanya vizuri, lakini hivi karibuni limetokea tatizo kwenye keyboard ya simu hiyo. Tatizo linasababisha kuonekana kwa matangazo unapotumia keyboard ya simu hiyo.

simu ya HTC 10

Mwishoni mwa wiki, mtumiaji wa Reddit, Azirack aligundua kuwa keyboard ya kwenye HTC 10 ilikuwa inaonyesha matangazo. TouchPal keyboard inaonekana ikionyesha matangazo kwenye sehemu ya juu ya keyboard, ikiwa ni pamoja na apps zilizowekwa ama unazoweza kuweka kwenye HTC 10. Toleo la bure la TouchPal kwenye vifaa vingine linaonyesha matangazo, lakini, hii sio nia ya HTC.

Kampuni hiyo imethibitisha kwenye Twitter kwamba kosa lisilofahamika limetokea na kusababisha watumiaji wa HTC 10 kuona matangazo kwenye keyboard ya simu hizo. Pia walisema kuwa wanafanya kazi ya kurekebisha na wanakusudia kutatua suala hilo kwa haraka kadri iwezekanavyo, lakini hawakutuhakikishia itachukua muda gani.

Getting random ads distributed via the keyboard, one of the most crucial elements of using a smartphone, would certainly be very annoying. It’s good to hear that HTC is working on a fix, though.

SOMA NA HII:  Njia rahisi kabisa ya kuroot simu yako ya Android

Kupata matangazo yanayo sambazwa kupitia kibodi keyboard, mojawapo ya vipengele muhimu zaidi vya kutumia smartphone, bila shaka itakuwa inakuboa. Ni vizuri kusikia kwamba HTC inafanya kazi ya kurekebisha, ingawa.

Je kuna mtumiaji yeyote wa HTC 10 amekutana na jambo hili?

Chanzo: Reddit, @HTC_UK

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.