AndroidMaujanja

Error 505: Tatizo la kushindwa kupakua apps kutoka Google Play Store

Umewahi kutana na neno ‘Error 505’ kwenye Google Play Store na ikasababisha ukashindwa kupakua apps kutoka Google Play Store ?

Tatizo la Google Play Store Error 505 linaweza tatuliwa kwa kutumia njia zifuatazo;

Njia ya Kwanza: Zima, washa na hakikisha muda wa saa

Zima na kuwasha simu yako. Muda mwingine kufanya hili tuu kunaweza ondoa tatizo hili na utaweza kupakua apps bila shida tena. Na pia hakikisha kama saa ya simu yako inaonesha muda ulio sahihi.

Jaribu kupakua app yeyote tena kupitia Google Play Store, ikikupa error ile ile tena nenda jaribu njia ya pili.

SOMA NA HII:  Mambo 6 ya Muhimu Kuzingati Kabla ya Kununua Simu Mpya

Njia ya Pili: Cache na Data za Google Play Store

Futa Cache na Data za Google Play Store

  • Nenda Settings
  • Bofya Apps au kwenye simu nyingine huwa panaitwa Application Manager
  • Bofya ‘All’ katika eneo la juu
  • Tafuta Google Play Store katika orodha na kisha ibofye
  • Hapa utaona machaguo mawili ‘Clear Cache’ na ‘Clear Data’, Bofya Clear Data kisha Clear Cache
SOMA NA HII:  Jinsi ya Kugawa Partition Kwenye Windows bila "Kuformat"

Njia ya Tatu: Akaunti ya Google

  • Nenda Settings
  • Katika eneo la Accounts bofya Google
  • Bofya kwenye akaunti yako ya Google na kisha bofya ‘Remove Account’
  • Zima simu yako na waishe tena
  • Fuata hatua za kuweka akaunti ya Google upya

Kama njia zote hizo zimeshindikana basi unaweza kufanya maamuzi mengine kama kureset simu yako. Ni matumaini yangu makala hii imekusaidia.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako