EFM imetimiza umri wa miaka mitatu. Kituo hicho cha redio kilichokua kwa kasi, kimekuwa kikitangaza habari mbalimbali za kijamii, kiuchumi, pamoja na michezo kwa lengo la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wasikilizaji wake.

Hadi sasa EFM imejitwalia tuzo ya ubunifu ya Tanzania Leadership Award kwa miaka miwili mfululizo, kwa kubuni matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakiiwezesha jamii kujikwamua kimaisha kwa kugawa pikipiki, magari ya biashara (shikandinga), fedha taslimu, maakuli (kapu la sikukuu) pamoja na mafuta kwa madereva wa vyombo vya usafiri pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wanawake.

Pia imeanzisha kampeni mbalimbali za kutia hamasa katika jamii ikiwemo (kampeni ya Mti wangu) yenye lengo la kumhamasisha kila mtu kupanda mti, na kufanya mazoezi mtaani pamoja wanafunzi wa vyuo kupitia kikundi cha Efm jogging club.

SOMA NA HII:  Je una bashiri "kubeti" ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?

Redio hii imejipatia umaarufu sana kwa kuukuza muziki wa Singeli ambao awali ulidharauliwa na kukosa hadhi. Licha ya kuukuza redio hii imeusafisha kwa kuwaelimisha wasanii wa muziki huo kwa kuwapa semina mbalimbali ikishirikiana na taasisi mbalimbali kama BASATA, COSOTA, TCRA, na TRA hadi sasa muziki huu unachezwa na kutambulika na redio nyingine ndani na nje ya Tanzania.

Aidha katika kuendeleza mafanikio yake, Redio hii imeongeza masafa yake katika mikoa tisa ya Tanzania bara ambayo ni Mwanza, Mbeya, Mtwara, Singida, Tanga, Tabora, Manyara (Babati), Kilimanjaro (Moshi), na Kigoma pamoja na kuanzisha rasmi kituo dada cha Televisheni kinachofahamika kama TV-E ambayo kwa sasa inafanya vizuri.

SOMA NA HII:  Swali la Siku: - Kati ya Vitu Hivi 3, Ni Kitu Gani Ni Ngumu Kwako Kuishi Bila Kukifanya?

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako