Sambaza:

Mwanamuziki Ed Sheeran ameshirikishwa katika mwendelezo wa filamu za Game of Thrones – kama mwanajeshi.

Nyota huyo wa muziki aina ya Pop, anaimba na pia kuzungumza kwa muda mfupi katika makala ya sasa ya filamu hizo ambayo sehemu ya kwanza ya makala ya sasa ilipeperushwa mapema leo.

Sehemu hiyo ambayo imepewa jina Dragonstone, ndiyo ya kwanza kwenye makala ya saba ya mwendelezo wa filamu hizo maarufu sana kutoka Marekani.

Uigizaji wa mwanamuziki huyo wa miaka 26 uliwagawanya mashabiki wake mtandaoni, baadhi wakifurahishwa naye na wengine kumkosoa.

Mhusika ambaye Ed ameigiza jina lake halijatajwa. Anaonekana akiimbia akiwa na watu wanaoota moto msituni.

Mhusika Arya Stark anayeigizwa na Maisie Williams anapopitia hapo akiwa kwenye farasi, anamwambia, “Ni wimbo mzuri huo, sijawahi kuusikia awali.”

“Ni wimbo mpya,” Sheeran anajibu.

Ed amefurahia kushirikishwa kwake kwa kupakia picha kadha katika akaunti yake mtandao wa Instagram.

Shabiki wake mmoja Kalynn alisema huo (kumuona Sheeran akiigiza) ulikuwa “wakati mwema zaidi kwangu maishani”.

Ed Sheeran/ Instagram

Ryan Kathleen Greene naye akaandika, “wakati mzuri sana kwamba nimekuwa hai”.

Lakini wengine hawakufurahishwa, na Vann hata alipendekeza Arya Stark alifaa kumuua mhusika aliyeigizwa na Ed.

Sehemu hiyo ya Dragonstone itapeperushwa tena Sky Atlantic na Now TV leo usiku.

Makala yatakayofuata ya Game of Thrones yatakuwa ndiyo ya kwisho. Filamu hizo zimewepo tangu 2011.

SOMA NA HII:  Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako