Nyingine

Dubai imeingia kwenye Guinness World Records kwa kuwa na magari ya polisi yenye kasi zaidi duniani

Jeshi la polisi la Dubai limepewa cheti na Guinness World Records kwa kuwa na gari za polisi zenye kasi zaidi duniani- -Bugatti Veyron — moja kati  ya supercars  14 zinazotumika na jeshi hilo.

Magari mengine ya jeshi hilo ni pamoja na Aston Martin One-77 ambapo ni gari 77 tu za aina hii zimetengenezwa na kuuzwa, Bentley Continental GT, Porsche Panameras na BMW i8s.

Rekodi ya awali ina milikiwa na jeshi la polisi la Italia kupitia gari la Lamborghini Gallardo LP560-4, ambayo ina kasi ya juu ya 230 mph (370 km / h).

Ila gari hizo za kisasa za jeshi la polisi la Dubai hazitumiki kuwafukuza waharifu Sheikh Mohammed Bin Rashid Boulevard, ama majukumu mengine mengi ya polisi. Ila, zinazunguka maeneo ya Dubai Mall na Jumeirah Beach Residence kutafuta watalii.

Ndio, unaweza kusimamisha gari la polisi na kupiga selfie na dereva ukiwa Dubai.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Tecno S1 na Bei yake Nchini Tanzania

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako