Sambaza:

Staa wa soka aliyewahi kuichezea Chelsea ya England kwa mafanikio Didier Drogba amerudi tena uwanjani toka aachane na timu ya Montreal Impact.

Staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 39 licha ya kuwa alipokea ofa nyingi kutoka katika timu za England, China, Ufaransa na timu ya Corinthians ya Brazil amekaa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa baada ya kuachana  na Montreal Impact aliyoichezea kwa miezi 18.

Leo Drogba ametangazwa kujiunga na timu ya Phoenix Rising FC ya Marekani iliyopo daraja la tatu (American’s United Soccer League) kama mchezaji na sehemu ya mmiliki wa timu hiyo ambayo sio maarufu.

SOMA NA HII:  Teknolojia 5 Maarufu kwenye Magari Kwa Sasa

Drogba ana malengo ya kuiwezesha Phoenix ishiriki Ligi Kuu Marekani (MLS) mkataba wa kuichezea timu hiyo unaweza kuwa wa misimu miwili au mitatu kabla ya kuamua kuwa kocha au sehemu ya utawala wa timu hiyo, Drogba ana hisa katika timu hiyo.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako