Gaming

Dondoo za kubeti idadi ya magoli

on

Mkakati wangu kwenye kubeti ni kubashiri magoli yaliyofungwa na timu. Napenda kubeti mpira wa miguu na wakati mwingine mpira wa kikapu. Niligundua baada ya muda mrefu wa kupoteza fedha kutokana na kuwa vigumu sana kuchagua timu itakayo shinda mojamoja. Badala yake, nikaanza kubeti idadi ya magoli (katika soka) na mara nyingi mkeka wangu hutoa vizuri,

Nimecheza kwa zaidi ya miaka 3 kwenye mpira wa 1, X, 2, na handicap lakini niligundua, hasa kwenye handicap kushinda ni vigumu sana. Mara nyingi nilipoteza. Naam, ilikuwa ngumu sana. Nilikuwa nikijaribu kupata habari zote kuhusu mchezo wa soka: majeruhi na kusimamishwa, kuangalia mechi ili kujua ikiwa timu ni bora au mbaya kutokana na msimamo wa sasa.

Hakuna nilichofanikiwa. Nilitumia muda mwingi ambao haukunisaidia kuchagua bet yangu kwa usahihi.

Sasa, mkakati wangu. Kama nilivyosema, niliona kwenye mechi za mpira wa miguu kuna kuwa na magoli mengi , hata timu za chini hupata magoli mara nyingi. Napenda kubet kwenye magoli kwa sababu binadamu hufanya makosa mara nyingi na magoli hufungwa mara moja baada ya makosa ya kujihami. Goli linaweza kufungwa hata dakika ya 90 na unaweza kushinda dakika ya mwisho ukiwa na bahati. Ninahitaji angalau wafungane magoli mawili ili kushinda.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kufurahia Zaidi Michezo ya Kubahatisha "Kubeti"

Rahisi kama hivyo. Sasa ninacheza 1.5 goals ingawa ni odds ndogo, lakini angalau ninashinda mara nyingi.

Kwa mkakati huu kufanya kazi, nina aina tofauti za odds zinazokubalika: 1.2 ~ 1.35. odds, zile ambazo ni chini ya 1.20 sizitumii kabisa kwa sababu hatari ni kubwa sana kwa malipo kidogo. Niligundua kuwa odds zinavyozidi kuwa kubwa zaidi, kwa mfano zaidi ya 1.35, nafasi ya kushinda inakuwa ndogo.

Napendenda odds kubwa kadri iwezekanavyo lakini kwa mkakati wangu 1.35 ni odds inayonitosha kabisa.

Jinsi ya kuchagua timu na kupanga mkeka:

A. Kwanza nachagua ligi ambayo timu huwa zinafungana magoli meng, kwa mfano Netherland, division 1,2 Austria 2nd league, au Japan League.

SOMA NA HII:  Utabiri wa mechi na kubeti Over / Under 2.5 kwenye mpira

Nachagua ligi ambayo kuna odds nzuri kwenye  “over 2.5 goals” ni nzuri sana na bado kuna kwa zaidi ya asilimia 50 wamefungana magoli zaidi ya 3. Hii inanionyesha kuwa ligi husika iko wazi.

B. Katika kila ligi kuna timu zinazopaki bus na zinazocheza mpira wa wazi. Nangalia takwimu za timu na kupata timu ambazo angalau 80% ya michezo yake huishia kuwa na magoli angalau  2 ya kufungana. Zingatia kuwa timu zote mbili angalau ziwe na 80% ya michezo iliyoisha angalau na magoli 2. Kawaida huwa nachagua timu za katikati kwenye msimamo ambazo hazihofii kupoteza.

SOMA NA HII:  Je una bashiri "kubeti" ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?

C. Naangalia taarifa kuhusu timu husika lakini hili sio muhimu sana kwangu kwa sababu mechi nyingi ninaziangalia kwenye tv au kwenye mtandao. Inapokuwa siku nzuri nachagua timu 4-5 kwenye kubeti kwa mkakati huu.

D. Mara baada ya kupata orodha yangu ya kubeti kwa leo, sikimbilii kuweka bets yangu. Ninatumia bookmaker ambayo inaruhusu kufanya live betting. Ninatafuta kama mchezo wangu unapatikana kwenye live betting. Kama upo napenda kusubiri dakika 10 baada ya mchezo kuanza kisha ninaweka bet yangu. Niligundua kuwa kwa mbinu hii ninapata odds nzuri. Ikiwa odds ilikuwa 1.2 kabla ya mchezo kuanza, baada ya dakika 10 ya kucheza odds huongezeka pointi chache.

Kila pointi ni muhimu.

Kwa mkakati huu nimefanikiwa kwa zaidi ya 85%. Faida sio kubwa lakini angalau ni mkakati wa ushindi.

About Benix Matrix

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.