Nyingine

Dkt. Mwele Malecela aula Umoja wa Mataifa Kuongoza vituo vya magonjwa Afrika

Dkt. Mwele Malecela aliyekuwa Mwanamke wa kwanza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR na kisha ‘kutumbuliwa’ baada ya kutangaza uwepo wa homa ya Zika nchini, sasa anakuwa Mkurugenzi wa Vituo vya kuzuia na kudhibiti magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.

Pia, Dk Mwele aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mpango wa Maalumu wa WHO wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Espen) na sasa atahamia kituo chake cha kazi Congo-Brazaville. Mradi wa Espen ulianza kutekelezwa mwaka 2016 hadi 2020 na una lengo la kumaliza magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwa kutoa vifaa tiba, elimu na dawa.

Watu mbalimbali wametuma salamu za pongezi kwa uteuzi huu.

Miongoni mwa waliomtumia pongezi ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Sikika, Irenei Kiria ambaye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter:

“Hongera Mwele kwa kupata nafasi hiyo ina maana ulipangwa kulisaidia Taifa letu ukiwa nje.”

Mwingine ni Mhadhiri wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo aliyeandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema:

“Nina furaha kwa uteuzi wa Dk Mwele kuwa Mkurugenzi wa WHO. Nahisi kusamehewa kwa kuikosoa Serikali baada ya kumuondoa NIMR.”

SOMA NA HII:  Marufuku Matumizi ya Takwimu za Kampuni ya Geopoll - Dkt. Mwakyembe

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.