Nyingine

Diamond: Hali ya muziki sio shwari nakushauri Shetta fanya ‘muzikisiasa’!!!

Diamond Platnumz amesema hali ya muziki sio nzuri na amemshauri Shetta kufanya nyimbo ambazo ndani yake zina masuala ya siasa kutokana hali ya muziki utawaliwa na siasa.

Baada ya kuachia wimbo wa ‘Acha Nikae Kimya’ wiki iliyopita, wimbo ambao umemletea matatizo makubwa katika mitandao ya kijamii hali iliyomfanya aombe radhi.

Jumapili hii muimbaji huyo amshauri Shetta kufanya muziki huo huku akimtaadharisha kwa mambo mawili.

“Shetta ndugu yangu, Najua unanionea gere mwenzako toka juzi insta imehamia Madale….na wewe unataka kuingia kwenye huu upepo wa #Mzikisiasa …we usijiulize ingia tu😁…maana mjini sasa hivi vingoma vya Mapenzi Vigumu…ikiwezekana jifanye hata unataka kumtolea Mahali Mange Umuoe…Kesho mji wote wako…..ila kuna mawili: Sentro au Matusi😅😅😅😅 – #SimbaMason,” aliandika Diamond Instagram.

SOMA NA HII:  80% watashindwa mchezo huu: ni Glass gani itajazwa kwanza?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.