Sambaza:

Ofisi za Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki kituo cha televisheni cha Star na cha redio cha Radio Free Africa (RFA) zimefungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa deni la Sh4.5 bilioni.

Ofisi hizo zimefungwa leo Alhamisi (Julai 13) na wakala wa TRA, Kampuni ya Sukah Auction Mart and Court Brokers ya jijini Mwanza.

 

Meneja Utumishi na Utawala wa Sahara Media Group, Raphael Shilatu amethibitisha kuwa ni kweli ofisi hizo zimefungwa sababu wana malimbikizo ya madeni yanayotokana na kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali.

Lazima tukiri kwamba mmeshuhudia TRA wamefunga maeneo yetu ya kazi na hii inatokana na malimbikizo ya kodi ambayo siyo ya sasa ni ya muda mrefu hata nyie waandishi wa habari mnajua kwamba kadri uwekezaji unavyokuwa mkubwa ndivyo gharama zinazidi kwenye uwekezaji. So, ilitulazimu kutafuta fedha kwenye mabenki ili tuweze kukidhi matakwa ya Serikali ya kuhama analogy kwenda Digatal.

“Niwatoe wasiwasi Watanzania na wapenzi wa Sahara hili ni jambo la muda lakini kampuni yetu inafanya jitihada kuhakikisha kwamba haya yanamalizika vyombo vyetu virudi hewani.” amesema Rafaeli Shilatu


TRA wamewaondoa studio wafanyakazi wote na kuifunga radio hiyo. Kwa sasa ukiwasha radio utasikia matangazo ya kiingereza ya BBC.

SOMA NA HII:  Ripoti : Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako