#DeleteFacebook Inazidi Kuwa na Nguvu, Sasa ni Zamu ya Gazeti la Playboy


Gazeti la maisha ya wanaume wa Marekani na burudani, Playboy siku ya jumanne usiku imetoa taarifa kwa vyombo vya habari kutangaza kujitoa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Imefuta akaunti zote za Playboy ambazo zinasimamiwa na kampuni hiyo.

Playboy inakuwa kampuni nyingine kujiunga na kaulimbiu ya #DeleteFacebook baada ya kashfa ya Cambridge Analytica, hii imekuja baada ya amri ya Elon Musk kuondoa kurasa za Tesla na SpaceX kwenye mtandao huo wa kijamii unaomilikiwa na Zuckerberg.

”The recent news about Facebook’s alleged mismanagement of users’ data has solidified our decision to suspend our activity on the platform at this time,” reads the statement. “There are more than 25 million fans who engage with Playboy via our various Facebook pages, and we do not want to be complicit in exposing them to the reported practices.”

Playboy hakika haina ushawishi mkubwa wa kitamaduni, lakini brand yake bado ina nguvu fulani kwa kizazi cha sasa. Unajua, wale ambao wanatumia Facebook. Mwaka 2014, Playboy ilisema kuwa Facebook ilikuwa sehemu yake kubwa ya kujitangaza. Bila shaka, hiyo ilikuwa baada ya gazeti hilo kuacha kuweka picha za uchi kwenye mtandao huu (walianza tena mwaka jana) ili kupata watu wengi zaidi kwenye mtandao wa kijamii.

Ni muhimu kutambua hatua zilizochukuliwa na Playboy, SpaceX, na Telsa, hata hivyo, bado wanapatikana kwenye Instagram, ambayo inamilikiwa na Facebook.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA