#DeadAndGone: Tovuti ya ExtraTorrent yaacha kupatikana.

NowPlaying T.I Dead and gone kwa sababu hicho ndicho kilichotokea kwa Extratorrent, mtandao wa pili kwa ukubwa duniani unaoruhusu watu kudownload bila malipo. Watu wakitembelea tovuti hiyo leo watakuta na ujumbe huu:

TorrentFreak waliwasiliana na mwendeshaji wa ExtraTorrent SaM ambaye alithibitisha kuwa ni kweli huu ndiyo mwisho wa tovuti hiyo.

“Ni muda muafaka wa kusema kwaheri,” alisema, bila kutoa maelezo zaidi.

 

Kwa maoni yangu, inaonyesha kwamba jambo hili limefanyika kwa hiari na kitu kinachofurahisha ni kuwa, kumekuwa na kujitolea kuzima tovuti nyingi za aina hii ndani ya wiki chache zilizopita. Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa ya kwa nini wanaamua kuzifunga. Sasa, mimi nadhani kuna mtu anaweka shinikizo kubwa kwa watu hawa na wao wanafanya hivyo ili kuepuka makosa ya jinai.

Pia ni muda wa sisi kukubaliana na ukweli:

 

Siku za “pirating” kwa urahisi zinahesabika. Zimekuwa zikishambuliwa pande zote, na fedha ipo kwajili ya kuendeleza vita kwa muda itakaochukua, hivyo zifurahia wakati bado zinaishi. Hatimaye, itakuwa vigumu, na hivyo kuwekewa sheria ngumu  ambazo zitafanya watu wengi wakate tamaa.

RIP Extratorrent.

#ChangesSongTo: End of the road by Boys 2 men.

One Response

  1. Amani May 27, 2017

Leave a Reply