Home Nyingine Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi

Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi

0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kufuatia kukaidi wito wa jeshi hilo alipotakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati kwa ajili ya mahojiano kufuatia tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amethibitisha taarifa hizo kuwa wanamshikilia kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na chama hicho, zinadaia kuwa Freeman Mbowe ameenda Kituo cha Polisi mwenyewe kuitikia wito.

Awali kiongozi huyo alisema kuwa hawezi kwenda kituo cha Polisi kwa sababu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hakuwa na mamlaka ya kumuita kituo cha polisi na pia kwa sababu taratibu za kumuita kituoni hazikufuatwa.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *