Nyingine

David Moyes matatani baada ya kumtishia kumpiga kofi ripota wa BBC

Baada ya kumtishia mwandishi wa BBC Vicki Sparks kwamba atampiga makofi , meneja wa Sundarland David Moyes yupo matatani baada ya Chama cha soka nchini England (Fa) kutangaza kuwa kitamuhoji.

Mwandishi huyo alimuuliza moyes uwepo wa mmiliki wa timu Ellis Short uwanjani unamletea wasiwasi wowote ndio kocha huyo akatoa maneno hayo ya vitisho.

Tukio hilo lilitokea tarehe 18 ya mwezi uliopita baada ya kumalizika mchezo wa wa ligi kuu England kati ya Sunderland na Burley . Hata hivyo tayari David Moyes amekwisha muomba radhi mwandishi huyo na kujutia makosa yake.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Moyes amekiri kujutia kitendo hicho,

“Nimekubali kosa.Nimeongea na Ripota wa BBC, ambaye amekubali msamaha wangu”. .

SOMA NA HII:  Nahitaji Antivirus, Je Wewe Unatumia Antivirus Gani Kwenye Kompyuta Yako?

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako