Sambaza:

Ripoti ya robo ya pili ya mwaka huu iliyotolewa na TCRA inakupa picha halisi  ya mtandao gani wa simu ni nafuu zaidi, na pia ukuaji wa mitandao hiyo.

TCRA

Mtandao wa Halotel na Airtel ndio wamekuwa kwa kasi zaidi katika miezi ya tano na sita mwaka huu kuliko mtandao mwingine wowote wa simu. Wakati Halotel walipata wateja wapya 218,588, Airtel walipata wateja 136,862, wakati Tigo walipata wateja 113,703 na huku Vodacom wakipoteza wateja 5,673.

Data za ukuaji wa wateja wapya.

Data zinazoonesha ukuaji kwa miezi ya tano na sita mwaka huu

SOMA NA HII:  Zitto Kabwe: Sakata la Airtel ni kama NBC
Je mtandao gani ni nafuu zaidi?
  • Gharama za maongezi – simu za maongezi

Wastani wa gharama za maongezi katika Tsh kwa kila dakika ya maongezi kwa simu za wateja wa mtandao huo huo – (bila kujiunga vifurushi)

Gharama kwa simu za kwenda mitandao mingine (mfano: mtu wa Airtel akipiga kwenda mitandao mingine). Bei ni kwa dakika (Tsh)

Gharama za SMS (UJumbe mfupi)
  • SMS za ndani ya nchi

Gharama za ujumbe mfupi (SMS) kwenda mitandao mbalimbali (nje ya kifurushi)

  • SMS kwenda nje ya nchi

Gharama za ujumbe mfupi kwenda nje ya nchi

Soko la huduma za kibenki za mitandao ya simu kufikia Juni 2017;

Ukuaji wa huduma za kibenki za simu

Mtandao wa Tigo ingawa ni maarufu sana umekuwa ni mmoja wa mtandao wenye gharama za juu sana. Ila unaonekana unaendelea kukua (umeshikilia nafasi ya tatu).

Halotel na Airtel wanaukuaji mzuri. Inaonekana nguvu ya ziada waliyoweka Halotel kuyafikia maeneo mengi mapya inawalipa, wameendelea kuwa na ukuaji mzuri kwa muda mrefu sasa.

Kwa ujumla wake mitandao yenye gharama nafuu zaidi hata kama mtumiaji hatumii kifurushi ni Halotel, TTCL, Smart na Zantel.

Airtel Money inaongeza kwa ukuaji ukilinganisha na huduma zingine za kibenki za mitandao ya simu, idadi ya watumiaji ilikuwa kwa asilimia 12 katika kipindi hicho. Ukuaji wake na ule wa TIgo Pesa unaonekana kupunguza idadi ya watumiaji wa M-pesa (Vodacom).

Je wewe una mtazamo gani juu ya matokeo haya? Unaweza kusoma ripoti nzima hapa – TCRA TelCom-Statistics-June-2017


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako