Apps za Simu

Dalai Lama azindua app ya bure kwajili ya watumiaji wa iPhone

on

Dalai Lama amezindua app ya simu kwa wafuasi wake kuweza kufuatilia kwa karibu kuhusu safari na mafunzo yake.

Kiongozi huyo wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni mwenye umri wa miaka 82, ana akaunti ya Twitter iliyo na wafuasi zaidi ya milioni 16.

App hiyo ya bure kwa sasa inapatikana kwenye simu za iPhone pekee, na ataitumia kutoa taarifa, video, picha na taarifa nyinginezo.

Kuna programu nyingi tumishi za kidini zilizozinduliwa, zinazoruhusu viongozi kuwasiliana na wafuasi wao na kuwasiaidia watu kutafuta chakula kinachoambatana na dini zao, wanaposafiri.

SOMA NA HII:  Tumia camera kupiga selfie, unapata majibu ya saratani

App hiyo inaitwa, Dalai Lama, haijakaguliwa sana na watumizi.

Dalai Lama

  • Jina lake ni Tenzin Gyatso
  • AlizaliwaTibet, amekuwa uhamishoni kwa miongo sita tangu Uchina ukandamize vuguvugu la Tibet
  • Yeye ni Budda, anayetambulika kama mojawapo ya viongozi wakuu duniani na huhubiri amani na uvumilivu wa ki imani mara kwa mara
  • Anashinikiza kujitawala kwa Tibet iliomo ndani ya China lakini utawala wa China unamuona kuwa mtu anayeshinikiza kugawanayika kwa nchi hiyo
  • Mnamo 1989 alishinda tuzo ya Nobel ya amani
  • BBC imeshinda kupata picha yake akiwa anatumia simu za kisasa ‘smartphone’

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.