Sambaza:

Habari marafiki zangu, leo tena nimeleta kwenu mada kuhusu uvaji wa mavazi yasiyofaa mbele y umma.

Imekuwa kama ni fashion siku hizi jinsi wanawake wanavyovaa mitaani, yani mwanamke anayeonyesha zaidi viungo vyake ndo anaonekana anavutia zaidi, mfano , hua nawaona wadada wengi sana wanavaa mini skirt fupi sana kiasi kwamba akiwa amesimama tu inaonyesha mpaka juu ya magoti yaani mapaja na hapo hujamcheki nyuma, utakuta hiyo hiyo mini skirt kaichana na mpasuo mkali.

Wanawake siku hizi wanaacha maziwa nje, mistari ya makalio nje, mapaja nje, wengine hawavai chupi, sidiria, wala skin tite. Si ajabu sasa kuuona uchi wa mwanamke mkiwa ndani ya daladala, ofisini, barabarani wakitembea, sehemu za starehe n.k

Muda mwingine najiuliza mavazi yanayovaliwa na dada zetu siku hizi ni fashion ama ni wazimu.

Sioni sababu ya wanawake kuvaa hivyo na kupiga picha kisha wanaweka kwenye mitandao ya kijamii.

Je kwako inaleta maana? Mada hii imekuwa ikizungumziwa sana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na nimeamua kuileta hapa Mediahuru tujadili kwa pamoja, je ni fashion wanawake kuvaa nusu uchi?

Hakuna shaka kuwa mitindo inatupeleka sehemu mbaya , kwa sababu mwanamke anaweza kuvaa nusu uchi mtaani na ukimuuliza atakwambia ndo mtindo mpya mjini.

Nini?

Fashion inakupa uwezo/mamlaka ya kuvaa nusu uchi mitaani? Dunia ya mitindo ipo kwenye moto kwa sababu kila siku nguo ambazo sio salama kuvaliwa na wanawake ndo zinatengenezwa sana .

SOMA NA HII:  Hali ni mbaya sana kwa tovuti za Pirates na wazee wa Torrent

Linapokuja swala la fashion wanaume hawajaachwa nyuma, ila uvaaji usiofaa wa hawa dada zetu kwa jina la fashion sasa ni out of control, na kunajenga historia mbaya kwa vizazi vijavyo .

Naomba niulize swali, kama bibi zetu enzi zao wangekuwa wanavaa kama wasichana wa siku hizi, unafikiri tungekuwepo hivi sasa? Ama unafikiri Dunia ingekuwa imeshakwisha mpaka sasa ?

Kwa hiyo nafikiri wanawake wanatakiwa kuangalia kwa jicho la tatu mavazi wanayovaa kulinda heshima yao kwa jamii.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako