BenkiHudumaHuduma za Mtandaoni

CRDB yazindua huduma ya Simu Account

Benki ya CRDB imezindua huduma mpya ya Simu Account kwa ajili ya kurahisisha huduma za kibenki kwa watumiaji.

Akizungumza leo Jumamosi, Agosti 26 wakati wa uzinduzi wa jukwaa la wanawake Dar es Salaam ambako pia huduma hiyo imezinduliwa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei amesema inalenga kuwafikia wananchi wote.

Amesema Simu Account ni mfumo wa utoaji huduma za kielektroniki kutoka CRDB ambao unamuwezesha Mtanzania yeyote kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi.

Dk Kimei amesema benki hiyo imeona fursa ya mkakati wa kuwakutanisha wanawake katika nyanja ya kiuchumi, hivyo ikawaletea huduma hiyo.

Amesema: “Ipo haja ya kuongeza tija kwenye benki ili tuweze kukua na kuwafikia Watanzania wengi.Ni asilimia 17 ya kati ya Watanzania 50 milioni ndiyo wanatumia huduma rasmi za kibenki.Katika takwimu hizo wanawake ni 25 milioni pekee.”

Hii inaashiria kuwa upatikanaji wa huduma hizi bado ni changamoto.

SOMA NA HII:  TBL Kujenga Kiwanda Kikubwa cha bia mkoani Dodoma
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako