Habari za Teknolojia

CIA imeonyesha “hard drives” za Osama bin Laden zenye video games, anime, na filamu za watoto

Miaka minne baada ya kuuliwa na jeshi la Marekani kwenye eneo lake nchini Pakistani, serikali ya Marekani imetoa orodha ya vitabu na makala zilipatikana nyumbani mwa Osama bin Laden. CIA ilitoa faili karibu 470,000 zilizopatikana kwenye hard drives zake, ambazo zinazoonyesha kuwa alikuwa anapenda michezo ya video (video games), sinema, video za YouTube, na anime.

Ukubwa wa faili zote unafika mamia ya gigabytes, lakini kumbukumbu imegawanywa katika makundi manne-sauti, nyaraka, picha, na video-ili kutafuta kwa urahisi. Kama unavyotarajia, CIA ilikuta taarifa vinazohusiana na ugaidi, kama vile mafunzo ya video, na journal ya Bin Laden, lakini pia kuna maudhui mengi ambayo hayakutarajiwa.

Baadhi ya filamu ni pamoja na Antz, Cars, Chicken Little, na Resident Evil. Pia kulikuwa na vitu vya kushangaza kama “emulated DS” kama vile New Super Mario Bros na Animal Crossing, pamoja na michezo ya PC ya Zuma Deluxe na Sniper Elite: Nazi Zombie Army 2, torrent kwajili ya Army Men 2, picha za Pac-Man na Perestroika Girls, Final Fantasy VII, na michezo mingine.


Inaonekana kwamba Bin Laden (au mtu katika nyumba yake) alikuwa shabiki wa anime, pia. Mfululizo mzima wa Devil May Cry series upo, video za animated kama vile Street Fighter 4: The Ties That Bind na Storm Rider – Clash of the Evils.

SOMA NA HII:  Vanessa Mdee amezindua ‘app’ ya simu ya Vee Money

Video za YouTube pia zinaonekana. Toleo la pili la kupakuliwa la nyaraka ya Septemba 11 ya Loose Change imeorodheshwa, pamoja na video za kushona mablanketi, soksi za watoto, na kofia. Pia kuna clip ya “Charlie bit my finger”. Nyaraka zingine zinazohusiana na nadharia za njama, ikiwa ni pamoja na faili za PDF kuhusu Illuminati, zilipatikana.

CIA inasema kwamba baadhi ya nyaraka, kama vile chochote kinachohusiana na usalama wa taifa, hazijawekwa wazi kwa umma. Malware na ponografia zilizopatikana zimefanywa siri.

Hapa kuna orodha ya vitu vyenye hakimiliki ambavyo vimezuiwa kutoka kwa umma:

 • Antz
 • Batman Gotham Knight
 • BBC Great Wildlife Moments
 • Biography – Osama bin Laden
 • Cars
 • Chicken Little
 • CNN Presents: World’s Most Wanted
 • Final Fantasy VII
 • Heroes of Tomorrow
 • Home on the Range
 • Ice Age: Dawn of the Dinosaurs
 • In the Footsteps of bin Laden – CNN
 • National Geographic: Kung Fu Killers
 • National Geographic: Inside the Green Berets
 • National Geographic: Predators at War
 • National Geographic: World’s Worst Venom
 • Peru Civilization
 • Resident Evil
 • Storm Rider – Clash of the Evils
 • The Kremlin from Inside (a documentary recorded from Al Jazeera)
 • The Story of India
 • The Three Musketeers
 • Where in the World is Osama bin Laden
SOMA NA HII:  Wema Sepetu na Jokate ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii #Tanzania Heritage Month

CIA imetoa angalizo kwamba licha ya kupitia maudhui, bado kuna baadhi ya maudhui “ni ya kusikitisha na / au yanavuruga kihisia”. Inaweza pia kuwa na programu hasidi ambayo wataalamu wa CIA hawajaiona. Kwa kuzingatia hayo akili, unaweza kuangalia vitu vya Bin Laden hapa.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako