Nyingine

Chumba cha kaburi la Yesu chafunguliwa tena

Chumba kidogo kinachofunika kaburi ambalo inaaminika Yesu Kristo alizikwa kimefunguliwa rasmi tena baada ya kufanyiwa ukarabati kwa miezi tisa.

Chumba hicho ambacho kinapatikana katika Kanisa la Kaburi la Yesu Kristo katika maeneo ya mji wa zamani wa Jerusalem kilikuwa kimeharibika na rangi yake ilianza kuwa nyeusi kutokana na masizi ya mishumaa ambayo huwashwa eneo hilo.

Mzozo kati ya madhehebu matatu ambayo kwa pamoja husimamia kanisa hilo – Kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, Kanisa la Kiarmenia na Kanisa Katoliki la Kirumi – ulichelewesha ukarabati huo kwa miongo mingi. Chumba hicho kilifanyiwa ukarabati mara ya mwisho mwaka 1810.

SOMA NA HII:  Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka Ubalozi wa China

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako