Home Nyingine Chege kutoa album yake binafsi kabla ya aliyofanya na Temba

Chege kutoa album yake binafsi kabla ya aliyofanya na Temba

0
0

Wakali WA bongofleva Chege na Temba kutoka TMK Wanaume Family wamefanikiwa kurudi tena wakiwa pamoja kwenye ngoma yao mpya ya Go Down waliyompa shavu Emmy Wimbo.

Umekuwa ni ujio ambao umewashtua wengi kwani ni muda mrefu tangu tusikie sauti za wakali hao zikiwa zimekaa kwenye mdundo mmoja.

Sasa kama umekoshwa na collabo hiyo ya wakali hao, kaa tayari kusikiliza midundo mingine mingi itakayopatikana kwenye album yao,kwani kupitia kipindi cha Supermega kinachoongozwa na Prince Ramalove kupitia Kings Fm,Chege ameweka wazi ujio wa album yao.

“Album itakuja lakini before album ya Chege na Temba, inatoka album yangu.Nafikiri wiki ijayo tutaiweka www.wasafi.com,” amesema Chege.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *