Maujanja

Fanya hivi ili Chaji ikae muda mrefu kwenye simu yako

on

Moja kati ya matatizo ya zama hizi kwa watumiaji wa simu ni uwezo wa simu zao kukaa na chaji. simu zinakaa na chaji kwa muda mchache kiasi kwamba inabidi wajinyime matumizi waache kufanya vitu fulani ili simu iweze kukaa angalau siku moja.

chaji

Mambo mengi yanachangia simu yako iwahi kuisha chaji, kwenye makala hii utapata elimu itakayo kusaidia kuyajua mambo muhimu zaidi ambayo yatasaidia kuongeza muda ambao simu yako inakaa na chaji.

Haya ni Mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kuongeza muda ambao simu yako inatumia chaji.

  • Punguza mwanga wa simu yako

Punguza mwanga wa simu yako mpaka katika kiwango ambacho unakihitaji, pia unaweza kuset simu yako kuwa katika Auto brightness kwenye simu za android kupata sehemu hii unaenda kwenye mipangilio (settings ) kisha unachagua display ambapo ukifungua ndani yake basi utakutana na sehemu ya kurekebisha mwana wa simu.

  • Funga Apps usizozitumia

Sitisha app ambazo hauzitumii, kama na wewe ni mvivu kuzima app mara unapomaliza kuzitumia basi jenga tabia ya kuizima na kuiwasha simu yako hii itasaidia kuzisitisha app usizozitumia.

SOMA NA HII:  Njia 6 za Jinsi Unavyoweza Kupunguza Matumizi ya Data kwenye Simu ya Android
  • Tumia “Battery saving Mode”

Kutumia¬†“Battery saving Mode” inafanya simu yako itumie chaji kwa kiwango kidogo sana, kwa sababu unapotumia mfumo huu simu yako hufunga apps zote zisizo muhimu na kuacha zile za muhimu tu zifanye kazi.

  • Zima “Data” wakati hutumii simu yako.

Watumiaji wa simu wengi (hasa watumiaji wapya) huwasha Data kwa bahati mbaya hii inapelekea simu zao kuisha chaji kwa kasi zaidi ya kawaida. Hakikasha kila wakati ambao hautumii Data basi iwe imezimwa katika simu yako maana nayo ni mchango mkubwa katika kumaliza chaji

  • Zima bluetooth

Bluetooth ni moja ya njia nyepesi za kurusha na kupokea mafaili lakini pia inapowashwa hutumia kiasi kikubwa cha chaji. Hakikisha bluetooth ya simu yako imezimwa kama haitumiki maana nayo huchangia sana kumaliza chaji ya simu.

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo unaweza kufanya ili chaji ya simu yako idumu kwa muda mrefu.

About Benix Matrix

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.