Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chdmiadema) kimenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kuzuia uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki kutokana na Bunge kukataa majina yaliyowasilishwa na chama hicho kwa ajili ya nafasi mbili za Chadema za wabunge wa Afrika Mashariki kwa madai kuwa chama hicho hakikuzingatia suala la jinsia.

Katika madai yao Chadema wamesema kanuni zinataka theluthi moja ya wabunge wote (9) wa jumuiya hiyo kutoka Tanzania na siyo kutoka kwa kila chama. Kesi ya msingi itataka tafsiri ya theluthi moja.

Maamuzi hayo yamefikiwa leo usiku na kikao cha wabunge wa Chadema waliokutana mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa msimamizi wa Uchaguzi Dr. Thomas D. Kashililah amesema Chama cha Chadema uteuzi wao haukuzingatia jinsia, lakini pia hawajaambatanisha fomu za maombi ya wagombea, orodha ya waombaji pamoja na fomu ya matokeo ya kura.

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako