Baada ya taarifa za Cambridge Analytica, Vyama vya upinzani nchini Kenya vinataka uchunguzi wa kampeni za uchaguzi


Vyama vya upinzani nchini Kenya vimeitisha uchunguzi kuhusiana na kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita, baada ya kampuni moja yenye makao yake jijini London, Cambridge Analytica, kudai kuwa ilihusika pakubwa na kampeni za uchaguzi ya zilizomfanya rais Uhuru Kenya kushinda mara mbili.

Kampuni hiyo ambayo imekana kutenda kosa lolote, pia inatuhumiwa kudukua data za kibinafsi za watumiaji milioni hamsini wa mtandao wa kijamii wa Facebook, ili kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2016 nchini Marekani.

Alexander Nix ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa Cambridge Analytica

Vyama vya upinzani sasa vinataka uchunguzi kuhusiana na kile walichokitaja kama habari za kupotosha ili kuhujumu nia ya Wakenya kabla ya uchaguzi mkuu.

Kamishna wa mawasiliano wa Uingereza anatarajiwa kuomba kupatiwa hati ya upekuzi mahakamani ili kufanya upekuzi kwenye ofisi za kampuni hiyo ya Cambridge Analytica ambayo ina makao yake jijini London.

Wakuu wa Kampuni hiyo walinaswa na chombo cha Channel 4 wakisema kuwa watatumia mbinu za kuvutia, na rushwa ili kuwaaibisha wanasiasa.

Cambridge Analytica imekana shutuma hizo.

Siku ya Jumatatu, Channel 4 ilirusha picha za kamera za siri zilizomuonyesha Mkurugenzi Alexander Nix akieleza mbinu za Kampuni yake ambazo angezitumia kuwafedhehesha wanasiasa mitandaoni.

Kwenye picha za kamera alionekana akipendekeza njia moja wapo ni ”kuwaahidi donge nono na kuhakikisha kuwa wanarekodiwa picha za video’.

Pia alisema anaweza ”kuwapeleka wasichana mpaka kwenye nyumba za wagombea” akiwasifia ”wanawake wa Ukraine ni warembo sana, mpango huo utafanikiwa vizuri sana”.

Bwana Nix aliendelea ”Ninawapa tu mifano ya yale yanayoweza kufanywa na yaliyofanywa”.

Hata hivyo,Kampuni hiyo imesema ripoti iliyotolewa dhidi yao na mazunguzo yaliyonaswa kwenye kamera ni ya ”uongo mtupu”

”Cambridge Analytica haijihusishi na vitendo vya rushwa wala mitego ya kushawishi” ilisema.

Nako nchini Kenya, Upinzani nchini humo umetaka Kampeni za mwaka jana za uchaguzi zifanyiwe uchunguzi baada ya Cambridge Analytica kusema kuwa zimeshiriki kuwa sehemu muhimu ya ushindi mara mbili wa Rais Uhuru Kenyata.

Upinzani nchini Kenya unataka ufanyie uchunguzi kile wanachodai kuwa Kampeni za kubadilisha matakwa ya raia wa Kenya.

Delano Kiilu, ambaye ni katibu mkuu wa chama cha kuhifadhi data, Protective and Safety Association of Kenya (PROSAK). amesema itabidi uchunguzi wa hali ya juu ufanywe kabla ya kuitia hatiani kampuni ya Cambridge Analytica.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA