Nyingine

CAG: Kuna udhaifu katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Ikiwa wakurugenzi sita, mameneja watano na mhandisi mmoja wamesimamishwa kazi tangu Julai mwaka jana kupisha uchunguzi. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini kasoro katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Ripoti hiyo iliwasilishwa bungeni Aprili 13, ikiwa ni siku chache tangu CAG, Profesa Mussa Assad aikabidhi kwa Rais John Magufuli.

Baada ya kufanya ukaguzi wa hesabu za Mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2015/16,  Kasoro zilozobainika katika mfuko huo ni kiwango cha chini cha ukaliwaji wa majengo, usimamizi na udhibiti wa mikopo ya vyama vya ushirika vya akiba na mikopo, udhaifu katika uwekezaji wa ardhi.

Ripoti hiyo inabainisha kasoro katika Shamba la Dungu na mradi wa uwekezaji Tuangoma, kasoro nyingine ni katika mkataba wa mshauri katika ununuaji wa Pan Africa Energy Limited kwa Sh551.61 milioni.

SOMA NA HII:  Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka Ubalozi wa China

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako