Makala

Blogger 4 waliuawa kwa sababu ya makala zao

Internet imekuwa chombo cha haki na mabadiliko. Kuna mamilioni ya watu wana  blog matatizo wanayokumbana nayo kama sehemu ya jamii , ni hakika baadhi ya watu hawa watajikuta kwenye matatizo (hata kuuawa) kwa sababu ya maandishi yao. Baadhi ya wanablogu hulipa gharama kubwa kwa maudhui yao. Kwa kweli, ni watu wengi zaidi pengine kuliko unavyofikiria.

Katika nchi nyingi, waandishi wa habari na wanablogu hudhibitiwa na kutishiwa na adhabu kwa kutaja kitu chochote kinachoikosoa serikali yao au nchi. Hata hivyo, wengi bado huhisi haja ya kuchapisha madai zao na kuongeza uelewa. Kwa bahati mbaya, baadhi ya waandishi hawa huuawa kwa sababu ya haja hii. Hebu tuangalie baadhi ya matukio ya hivi karibuni ya wanablogu ambao waliuawa kwa sababu ya maudhui yao.

U.S. Bangladeshi Blogger, Avijit Roy

Avijit Roy alikuwa anajulikana  kwa kuzungumzia secularism. Katika blogu yake, Free Mind, alikuwa anapingana sana na waislamu wenye msimamo mkali. Maandishi yake yaliwaudhi watu wengi wenye msimamo mkali katika dini hiyo, hasa wale walio katika nchi ya nyumba kwao Bangladesh. Ilikuwa ni Febraury 2015, wakati yeye na mke wake wametembelea Bangaladesh kwa ajili ya tukio la chuo kikuu. wanandoa walikuwa wakitembea kutoka kwenye book fair, walipo vamiwa na wapiganaji. wanandoa alishambuliwa na Roy alichinjwa  mpaka kifo. Mke wake pia alijeruhiwa katika shambulio hilo. 

Wakati bado haijawekwa wazi ni nani alihusika na kifo chake, polisi ilieleza BBC kwamba walikuwa wana fanya uchunguzi kuhusu kundi flani kidini. Kundi hilo lilipost na kupongeza mauaji hayo mtandaoni.

Ahmed Rajib Haider

Mauaji ya Roy yalitukumbusha kifo cha blogger mwingine , Ahmed Rajib Haider mwaka 2013. Haider alikuwa blogger mwingine kutoka Bangladesh. Sawa na Roy, Haider alichinjwa mapaka kifo na wanafunzi wa chuo ambacho kimekuwa na siasa kali na msimamo mkali wa Kiislamu. Kwa bahati nzuri, wauwaji wawili wenye mapanga walio fanya washambuliaji hilo walitambuliwa na kukamatwa. Wote wawili walihukumiwa kifo Desemba 2015, miaka miwili baada ya mauaji ya Haider. Mamlaka zilieleza kuwa Haider aliingia kwenye matatizo baada ya kuandaa maandamano dhidi ya viongozi wa Kiislamu.

SOMA NA HII:  Mfahamu Mwanzilishi Wa Kampuni ya Simu za Tecno - Tecno Mobile

Tangu vifo vya wanablogu hawa wawili kutoka Bangladeshi , wanablogu wengine watano wameuliuawa nchini humo.

Xulhaz Mannan na Mahbub Tonoy

Stori nyingine ya mauaji ya mwanablogu katika nchi ya Bangladesh. Wakati huu wanaharakati hawa hawakulengwa kwa sababu ya maandamano yao dhidi ya Uislamu, wakati huu ni kwa sababu ya upendeleo wa kijinsia. Mannan na Tonoy walifahamika zaidi kwa kuunga mkono haki za mashoga. Mannan alikuwa mhariri maarufu wa chapisho la jinsia. wanandoa walishambuliwa na kuuawa na washambuliaji waliovunja na kuvamia ya nyumba ya Mannan.

Kundi linahusishwa na Al-Qaeda haraka walisema wana husika na mauaji hayo, licha ya vitisho kutoka kwa waziri mkuu wa nchi hiyo kwamba adhabu itakuwa ni kali.

Katika matukio yote, familia za wahanga zilipigania haki. Ni muhimu kutambua kuwa wanablogu wanalengwa na hata kuuawa duniani kote, hata katika nchi ya Marekani. Wakati mifano yote hii ilitokea katika nchi ya Bangladesh, ni muhimu kutambua kwamba matukio mengine yamefanyika kimataifa. Wataalam wa sheria duniani kote wanaeleza kwamba kama blogger au mwandishi anahisi kutishiwa au kama familia ya marehemu inatafuta haki, ni muhimu mara moja kutafuta msaada. Pia, siku zote chukua tahadhari wakati wa kuandika kuhusu mada nyeti. Inawezekana kufikisha ujumbe wako huku ukijilinda mwenyewe.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako