Je Blog ni Nini na Jinsi ya Kutengeneza Blog?


Kuna watu wengi ambao bado hawajui blog ni nini au kwa nini “blogging” inazidi kupanuka katika ulimwengu wa wavuti. Nafikiri watu hawa wanastahili haki ya kujua blogu ni nini na jinsi ya kutengeneza blog pamoja na maswali mengine yanayofanana. Hivyo kwa wale ambao wamesikia tu neno Blog kutoka kwa marafiki zao, vyombo vya habari au chanzo kingine chochote, haya ni maelezo na mafunzo mafupi na sahihi ya kukusaidia kupata majibu ya maswali manne muhimu katika akili ya watu wengi.

Ambayo ni,

  1. Blog ni nini?
  2. Naweza kutengeneza Blog?
  3. Blog ina faida gani ?
  4. Blogger au WordPress ni nini?

Sasa hapa yanakuja majibu muhimu kwa maswali yote yanayoulizwa na watu wengi kuhusu blog

Blog ni nini?

Blog ni tovuti yenye maingizo yanayoitwa machapisho (posts) ambayo huonekana katika kwa utaratibu wa kutangulia chapisho jipya kwanza na kufuatiwa na machapisho ya nyuma. Kwa mfano kama juzi, jana na leo umeandika machapisho na kuyachapa katika blog yako basi katika kurasa yako ya mbele litaonekana kwanza chapisho la leo kisha la jana na kisha la juzi. Blog huhusisha makala unazochapa (machapisho), viungo (links) na maoni (comments) ya watembeleaji ili kuongeza maingiliano ya kimawasiliano kati ya blog na watembeleaji blog hiyo. Kwa kawaida blog huumbwa kwa programu maalum za kuchapishia.

Blogu sio kitu ila ni “Online Notebook Diary”. Tunaandika nini katika “diary” zetu? Bila shaka mambo ambayo tunayapenda na mambo tunayojisikia kuwa muhimu kuandikwa na kushirikiana na marafiki na familia zetu. “Diary” inaweza kuhusu mada yoyote unayopenda kwa mfano unaweza kuandika juu ya shughuli zako, mashairi, nyimbo, mafunzo, wanyama wa nyumbani, nyumba na familia, mawazo yako binafsi nk. Watu watasoma Diary yako ya mtandaoni kila siku na kuacha maoni.

Ikiwa unaandika juu ya uzoefu wako binafsi katika daftari la kawaida au karatasi, basi maandiko yako yatawafikia watu wachache tu ambao wapo karibu nawe lakini kwa gazeti la mtandaoni kama Blogu unazungumza na ulimwengu!

Kwa hiyo blogu ni tovuti yako ya kibinafsi ambapo unaandika na kushirikisha mambo unayopenda kwa mamilioni ya watu huko nje ambao wana hamu ya kusoma nini kinachopikika katika akili yako!

Naweza kutengeneza Blog?

Kutengeneza blogu ni bure kabisa. Kuna aina nyingi za huduma za uhifadhi wa Blogu (Blogging hosting services) ambazo unaweza kuchagua kuunda blogu lakini bora kati yao ni Blogger. Nimeunda nyingi kupitia Blogger bila hata kulipa pesa! Unataka kujua jinsi gani? Soma makala hapa chini juu ya jinsi ya kuanzisha blogu? !
Tengeneza Blog Bure kwenye Blogger.

Blog ina faida gani ?

Wewe hulipa chochote Badala yake Unapata $$ !! Unalipwa kwa kuonyesha matangazo kwenye Blogu yako. Watu wanapata $ 100 hadi $ 100,000 kila mwezi! Sitanii mfano ni problogger.net, TechCrunch na mashable.

Zaidi utakutana  na marafiki wapya katika ulimwengu wa Blogu na utapata heshima machoni mwa maelfu ya watu. Unaweza kuwa mtu Mashuhuri! Lakini yote haya kwa kazi ngumu kidogo na uvumilivu mkubwa.

Na faida nzuri ambayo nimeiona ni kwamba unajifunza kila dakika kwenye mtandao! Uwezo wako wa kutumia mtandao na kompyuta utaimarika kwa kiwango kikubwa na hii ndio nafasi ya kuonyesha mambo makubwa kutoka kwako. Kila dakika kwenye blogu bila shaka ni uzoefu mpya! Nimejifunza HMTL, CSS, XML na Javascript kidogo bila kwenda darasa lolote. Nilijifunza yote ndani ya mwaka wa kazi yangu ya “blogging” na leo nina uwezo wa kutengeneza template ya blogger bora katika masaa chini ya matatu MashAllah!

Blogger au WordPress ni nini?

Haya ndio majukwaa makuu ya blogu ambayo yanakusaidia kujenga Blog ya bure. Lakini ikiwa umechanganyikiwa na hujui utumie ipi basi anza na Blogger. Ina sifa nyingi ambazo wordpress haina na kitu kizuri ni kwamba Blogger inakuwezesha “KuCustomize template” yako kwa njia yoyote unayopenda kwa kuhariri karatasi ya mtindo Wa CSS (CSS style sheet) ! Sasa unatafuta nini? Tengeneza blogu yako sasa na uanze maisha mapya. Kila la heri!

Jisikie huru kuuliza swali lolote ambalo linasumbua akili yako.

2 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

    1. Ndugu blogger ni huduma ya bure kutoka google inayokuwezesha kuanzisha blog yako na kuweka machapisho yako ambayo watu kutoka pande zote za dunia wanaweza kuyasoma.

      Unaweza kujiunga na blogger kwa kutembelea tovuti yao ya blogger.com

ZINAZOHUSIANA