Sambaza:

Watanzania wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kununua na kuuza bidhaa, ili kupata unafuu wa bei na kuokoa muda wa kwenda kuzitafuta.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia nchini, Nina Holmes wakati kampuni ya kimataifa inayohusika na biashara ya mtandao Africa Internet Group ilipokuwa ikifanya uzinduzi wa mtandao wa Jumia Tanzania usiku huu baada ya kujikita Afrika kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Holmes alisema Jumia ni kampuni ya kimataifa inayohusika na uuzaji wa bidhaa mtandaoni, lakini pia inatoa nafasi kwa maduka na kampuni kuweza kuuza bidhaa zao kwa njia ya mtandaoni na inaweza kujitangaza bila kutumia gharama.

Amesema Tanzania ni moja ya kitengo kati ya vitengo kadhaa vilivyopo barani Afrika ikiwamo Jumia Nigeria, Jumia Kenya, Jumia Uganda.

Amesema vitengo hivyo vimefanikiwa kukuza biashara ya mtandaoni kwa kiwango kikubwa.

“Jumia ni biashara ya saa 24, muda wowote wateja wanaweza kuagiza chochote, kwa Jumia bila kujali muda wa kufunga au kufungua duka.

“Hii ni biashara ambayo imeenea karibu mikoa yote Tanzania,” amesema.


Sambaza:
SOMA NA HII:  Makosa 6 ya kifedha yanayofanywa na wamiliki wa biashara mpya na jinsi ya kuyaepuka

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako