BenkiBiasharaHabari za Teknolojia

Benki ya CRDB Kutumia Namba ya Simu Kufungua Akaunti

Baada ya kuwawezesha wateja wa benki hiyo kuhamisha fedha kwenda kwenye simu zao za mkononi, mfumo unaorahisisha kulipia bili za aina tofauti.

Mabadiliko ya mfumo wa kibenki na kukua kwa teknolojia kumepelekea Benki ya CRDB kukamilisha mchakato wa kuwawezesha wananchi kufungua akaunti kwa kutumia namba zao za simu za mkononi.

Benki ya CRDB Kutumia Namba ya Simu Kufungua Akaunti

Mpango huo umebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk Charles Kimei na kufafanua kwamba hizo ni juhudi za kuwawezesha Watanzania kufurahia huduma zao.

“Teknolojia inarahisisha kila kitu. Wateja wetu kwa sasa wanaweza kuhamisha fedha kwenda kwenye simu zao, kulipia bili za aina tofauti. Baada ya muda mfupi wataweza kufungua akaunti kwa simu zao,” alisema Dk Kimei wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo mjini Chakechake, Kusini Pemba.

Please subscribe to our newsletter

SOMA NA HII:  AFRIKA SASA ISIMAME KWA MIGUU YAKE
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako