Bei ya vifurushi vya intaneti inapanda kila siku. Yaani kwa sasa hivi kifurushi cha bei ya chini kabisa cha intaneti kwa mitandao karibu yote cha shillingi 500 unapata chini ya MB 100 iwe ni Zantel, Vodacom,Tigo, Airtel ama Halotel bei ni zile  zile.

Bei ya vifurushi vya intaneti

GB 1 kwa siku sasa hivi inauzwa kuanzia shillingi 2,000 kwenda juu, na ukinunua Kifurushi chochote cha kawaida tu unapewa Mb 1 hadi 10 kwa mitandao tofauti hata kama ungenunua cha mwezi ujazo wa data unakuwa unafanana wakati zamani kwa shillingi 500 ukijiunga na kifurushi unapewa dakika, sms na data mb 100, lakini siku hizi sijui hata nini kimetokea.

Ukitafuta sababu mtandaoni hutapata majibu ya moja kwa moja kwa sababu hakuna sababu maalumu ya kwanini vifurishi vinapanda bei kila siku zaidi utakutakana na nukuu tu zinazodai kuwa kodi wanazotozwa ndizo zinazofanya wapandishe bei na wao.

SOMA NA HII:  Vodacom yarudisha mtaji, Hisa zarejea bei ya awali

Nafikiri bundle zingekuwa na bei nafuu, kila mtu angekuwa ananunua na hii inamaanisha makampuni yangepata faida zaidi. Lakini kwa mtindo huu, wanaonunua ni wachache na bundle tunazonunua haziendani na thamani ya hela tunayotoa na wala hazitoshi kwa matumizi ya smartphone zetu ambazo ni kubwa na zina application nyingi.

Tuandikie maoni yako juu ya mada hii, Je watu wengi kutumia intaneti kufanya mawasiliano kuliko huduma za kawaida za simu (kupiga simu na kutuma sms) imesababisha vifurushi vya intaneti kupanda bei ?

Tuambie unahisi gharama za intaneti zitakuwaje utakapofika mwaka mwingine wa fedha ? Je zitashuka ama zitaongezeka zaidi?

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako