Sambaza:

Tecno imeendelea kusimama katika soko la smartphones kwa utoa simu nzuri tena kwa bei nafuu Zaidi ukilinganisha na makampuni mengine kama Samsung na HTC na inasemekana imechukua 50% ya soko la simu Afrika kwa sasa.

Tecno Phantom

Katika matoleo yake ya hivi karibuni ya Tecno Phantom 5 na lile la Tecno Camon C8 inaonekana kampuni hii imeamua haswa katika kujikita katika uzarishaji wa simu za kisasa na zenye ubora sawa na ule wa makampuni makubwa ila kwa bei rahisi Zaidi.

Tecno Phantom 5 ni simu ya kiwango cha juu kutoka kampuni ya Tecno.

Muonekano wa Tecno Phantom 5

Tecno Phantom 5 inakuja na kioo cha ukubwa wa inchi 5.5, kioo kikiwa ni cha teknolojia ya vioo vigumu vya Gorilla Glass toleo la 3. Hii ina maanisha kioo hakitachubuka au kukwanguka kirahisi, ni kigumu kuvunjika pia.

SOMA NA HII:  Njia bora ya kuroot simu yoyote ya tecno bila kutumia kompyuta

Cha kusifiwa kwa Tecno kwenye Phantom 5 ni pamoja na uamuzi wa kutumia chuma (Metal) katika simu hiyo. Hii inaleta utofauti ikilinganishwa na simu zingine ambazo majumba yake (housing)

Inakuja na kamera mbili, ya selfi ni ya megapixel 8 na inakuja na uwezo wa flash pia, wakati kamera ya nyuma ni ya megapixel 13.

Nyuma pia kuna sensor spesheli ya kusoma alama za vidole – ‘Fingerprint scanner‘. Kupitia hii basi hautaitaji kuingiza nywila (password) kwa kuandika, utaweza fungua simu yako mara moja baada ya kugususha kidole husika kwenye scanner hiyo.

Pembeni ina maeneo ya kuzima na kuwasha, pa kuongezea sauti na pia sehemu ya kuchomeka memori kadi na pia sehemu ya kuweka laini za simu (mbili).

Kamera yake

Phantom 5 inakuja na kamera yenye kiwango cha juu katika eneo la Megapixels, hii ikiwa ni Megapixel 13 kwa kamera ya nyuma na megapixel 8 kwa kamera ya selfi na hizi zote zikiwa na uwezo wa kutoa mwanga wa ziada (flash).

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Infinix Zero 5 bei na Sifa zake

Vipengele vingine vya Tecno Phantom 5

Laini mbili: Kuna wengi ambao bado wanaona umefikia muda wa Tecno kutoa matoleo ya laini moja pia kwa baadhi ya simu zao za hadhi ya juu kama matoleo ya Phantom. Phantom 5 inakuja na uwezo wa laini mbili, (Micro).

Inatumia Programu endeshaji ya Android, toleo la 5.1 Lollipop… na uchunguzi wa haraka haraka unaonesha kuna uwezekano watumiaji wake wakapata sasisho (update) ya kuwapeleka Android 6.0 – tutachunguza zaidi kuhusu hili, kama ni la kweli basi ni habari njema.

Inakuja na diski uhifadhi wa GB 32, ila utakutana na nafasi ya takribani GB 25 za kutumia. Nafasi ya kutumia memori kadi (Micro SD) kunakupa uwezo wa kuweka kadi ya hadi kufikia GB 128

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Itel S32 na Itel S32 LTE bei na Sifa zake

Inakuja na kiwango cha RAM cha kutosha, hii ikiwa ni cha GB 3 na hii itasaidia kuhakikisha hakuna apps zinazokuwa nzito pale unapoitumia.

Sifa zingine;

  • Inakubali hadi teknolojia ya 4G LTE (EDGE, 3G, 4G)
  • Display – Inchi 5.5, Pixels 1080 x 1920 (401 PPI), HD, Gorilla Glass 3
  • Aina ya prosesa: 64 Bit Octa-core 1.3 GHz CPU (Mediatek MT6753)
  • Prosesa ya Graphics – Mali-T720 (Hii itasaidia kufanya ubora wa vitu kama uchezaji magemu uwe mzuri)
  • Betri la kutochomoa; mAh 3,000
  • Pia teknolojia zingine zote muhimu zinapatikana kama vile Bluetooth, Hotspot (Tethering), WiFi n.k

Kutegemeana na ulipo na wauzaji husika, bei ya Tecno Phantom 5 ipo kati ya Tsh 700,000 hadi 800,000 .

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako