Bei ya Simu za Tecno Tanzania


Simu za Tecno zinazidi kuwa maarufu miongoni mwa watumiaji, simu za tecno bei zake huwa nafuu na ni nzuri kwa watu ambao wanahitaji simu zenye teknolojia za kipekee kwajili ya watu wa daraja la kati na matajiri nchini Tanzania. Kwa bei chini ya Tsh 60,000 mtu anaweza kununua simu ya Tecno inayotumia Android, hii inafanya iwe moja ya kampuni kubwa za kuuza simu zinazopendwa na vijana nchini Tanzania.

Simu za Tecno & Android

Tecno ilianza kutengeneza simu za bei nafuu na feature phones, lakini baadaye ilianza kutengeneza simu za Android. Kutengeneza simu za mkononi kwenye jukwaa lililojaribiwa na linaloaminika la Android na kuuza bei ya chini imeongeza umaarufu wa simu za Tecno nchini Tanzania na Afrika nzima.

Baadhi ya vitu vinavyozungumzwa sana kuhusu Tecno ni simu zao za Android. Hapa utapata simu bora za Tecno katika soko la Tanzania pamoja na sifa na bei zake.Pia tunaangalia matoleo ya Android, kwa sababu ni simu za Tecno bora zaidi.

Tecno Boom J8

Tecno Boom J8 ni miongoni mwa simu za mkononi za Tecno kwajili ya muziki ina nguvu na gharama nafuu. Boom J8 inakuja na kioo cha HD inchi 5.5 na screen resolution ya 1280 x 720 pixels. Kwenye kamera, Boom J8 inajumuisha kamera ya nyuma ya mexapixels 13 na LED flash na kamera ya mbele ya megapixels 5.

Kwa kuwa na quad-core MediaTek MT6753 processor, unaweza kutarajia utendaji mzuri kutoka kwenye smartphone hii ya kiwango cha kati.

Inapatikana Kwenye duka la Tecno kariako, bei yake ni TSH 200,000 – 250,000 Inategemea na Utakapo Nunua.

NUNUA BOOM J8 KWA TSH 200,000

Tecno Camon C5


Tecno Camon C5 ilikuwa simu janja ya kwanza ya Tecno kuwa na uwezo wa 4G LTE na ni moja ya simu ya bei nafuu inayounga mkono teknolojia hiyo.

Tecno Camon C5 ina kioo cha 5-inchi, kamera ya nyuma ya MP 8 na kamera ya mbele ya 2MP. Simu hii inatumia Android 5.0 (Lollipop) na inawezeshwa na 1.3GHz quad-core processor na 1GB ya RAM. Bei yake inaanza karibu na Tsh 200,000.

NUNUA TECNO CAMON C5 HAPA

Tecno Camon C8

Unatafuta chaguo la bei nafuu la Camon C9? Hapa kuna toleo lake dogo, itafanya unachotaka ingawa si kama C9. Lakini kwa bei yake nzuri, ni nani anayejali?

Camon C8 ni simu ya kushangaza, ina kamera ya 8MP nyuma, Watumiaji wanaweza kuchukua matukio kama yalivyo. Kamera ya mbele ina 5MP ni kwa mashabiki wa selfie.

Ikiwa unatafuta simu ambayo si ya gharama na inaweza kufanya chochote unachotaka kwa kuridhisha, basi Camon C8 ni simu ya kununua. Soma uchambuzi/mapitio kamili na uwezo za Camon C8.

Inapatikana Kwenye duka la Tecno kariako, bei yake ni TSH 200,000 – 270,000 inategemea na Utakapo Nunua.

NUNUA TECNO CAMON C8 HAPA

Tecno W4

Tecno W4 ni mtangulizi wa W5. Kwa hiyo, W4 ina uwezo gani ikilinganishwa na W5?

Utastaajabishwa W4 ina sifa nzuri na vipengele vinavyopendekezwa. Maneno kwenye mtandao ni kwamba, Tecno w4 ni simu ya kwanza ya kutumia Android 6.0 Marshmallow. Angalia uchambuzi kamili na bei ya Tecno W4.

Inapatikana Kwenye duka la Tecno kariako, bei yake ni TSH 140,000 – 170,000 inategemea na Utakapo Nunua.

NUNUA TECNO W4 HAPA

Tecno L8

Hakuna simu ya Tecno kwenye soko ambayo ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi betri kama L8, ina 5050 mAh, betri ina uwezo wa kukaa siku nzima hata wakati wa kucheza michezo ya HD, kuvinjari, na vitu vingine.

Tecno L8 ilitoka pamoja na Tecno W4. L8 ni mrithi wa Tecno L7, na kama vile ilivyokuwa na mrithi wa simu, L8 inakuja na ubora wa kamera, hifadhi ya betri, na maboresha mengine.

Inapatikana Kwenye duka la Tecno kariako, bei yake ni TSH 150,000 – 240,000 inategemea na Utakapo Nunua.

NUNUA TECNO L8 HAPA

Tecno J5

Tecno Boom J5 ni mrithi wa Tecno J7 ya ajabu. Ina kioo cha 4.5-inch, kamera ya 5MP nyuma na kamera ya 2MP mbele.

Tecno J5 ni maalum kwa wapenzi wa muziki na burudani. Inatumia Android 5.1 (Lollipop) kwenye 1.3GHz quad-core processor na 1GB ya RAM.

NUNUA TECNO J5 HAPA

Tecno Y6

Hii ni simu ya bei nafuu kutoka Tecno na ina sifa ambazo zinaweza kukushangaza kutokana na bei yake. Tecno Y6 ina skrini kubwa ya IPS 5-inch, dual-core processor na betri yenye nguvu ni kati ya sifa zingine za kuvutia.

Tecno Y6 haina tofauti sana na kile unachotarajia kwenye simu janja ya bei nafuu kutoka kwenye kampuni hii. Imetengenezwa kwa plastiki na ni nyembamba kiasi (10.6 millimetres).

Ina skrini ya ikubwa wa inchi 5 (resolution 854 x 480 pixels) – kiwango kipya kwa simu za bei nafuu. Pia kioo chake kinatumia teknolojia ya in-plane switching (IPS).

NUNUA TECNO Y6 HAPA

Tecno Phantom 5


Tecno Phantom 5 ni mrithi wa Tecno Phantom Z, ikiwa na kioo cha HD chenye 5.5-inch, 3GB ya RAM, fingerprint sensor, 4G LTE ya haraka, na inakuja na Android 5.1 Lollipop. Ingawa toleo la Android limeboreshwa kuwa Android 6.0 Marshmallow.

NUNUA TECNO PHANTOM 5 HAPA

Simu Zingine za Tecno

Hapa kuna Simu nyingine za Tecno unazoweza kununua. Baadhi yake zinaweza kuwa hazipatikani tena nchini Tanzania

Orodha hapo juu ni simu za Tecno bora zaidi nchini Tanzania. Tecno imetoa simu nyingi sana nchini Tanzania hizi hapa ni baadhi tu.

Hata hivyo kwa sababu simu za Tecno ni za bei nafuu zinaweza pia kuwa na changamoto zote zinakuwa kwenye simu za bei nafuu za Android kutokana na vifaa vyenye uwezo mdogo kama vile maisha mafupi ya betri , utendaji usiovu, nk.

Lakini kama unahitaji simu tu ambayo inafanya kazi, Simu za Tecno zitakufaa sana.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA