Nyingine

Bei ya dizeli, mafuta ya taa yapanda, Petroli yashuka

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA) imetangaza mabadiliko ya bei za mafuta.

Bei ya rejareja ya Mafuta ya Taa nchini imepanda kwa Shilingi 7 mwezi huu huku petrol ikishuka kwa shilingi 3 kwa lita.

Bei ya Dizeli imeongezeka kwa shilingi 12 kwa lita sawa na asilimia 0.36 kutokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei pia gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa bei ya rejareja ya petroli imepungua kwa shilingi tatu kwa lita moja sawa na asilimia 0.13, huku bei ya jumla ikishuka kwa Sh 5.65 kwa lita au asilimia 0.29.

Wakati petroli ikishuka, bei ya dizeli imepanda kwa Shilingi 12 kwa lita moja sawa na asilimia 0.63, bei ya jumla imeongezeka kwa Shilingi 9.11 kwa lita sawa na asilimia 0.50.

“Bei ya rejareja ya mafuta ya taa imepanda kwa Sh saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 ambako bei ya jumla imepanda kwa Sh 3.68 kwa lita sawa na asilimia 0.21.”

“Kwa kiasi kikubwa, mabadiliko haya ya bei yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei na gharama za usafirishaji (BPS Premiums) ikilinganishwa na mwezi uliopita,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha Kaguo ametoa rai kwa wafanyabiashara  kuwa huru kuuza bidhaa za mafuta ya petrol kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo ziwe chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa kulingana na kanuni ya kukokotoa bei za mafuta iliyopitishwa na EWURA.

SOMA NA HII:  Kwa nini Mwanamke Anaweza Kuweka Picha Zake Za Uchi Kwenye Simu Yake? - Uzoefu Binafsi

Pia EWURA imevitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

Kaguo amewataka wanunuzi wanapata stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.