Nyingine

Basi lenye Wanafunzi laua wanafunzi na walimu (karibu wote) Arusha (+ Picha)

Asubuhi ya leo imeripotiwa ajali mbaya iliyotokea Mlima Rohotia, Karatu mkoani Arusha ikuhusisha basi la Wanafunzi ambao walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema.

Taarifa za awali zinasema kuwa Dereva wa basi la wanafunzi wa Shule ya LackVicent alishindwa kuliongoza vizuri basi hilo wakati akikata kona kwenye mteremko hivyo likaingia kwenye korongo

Kamanda wa Polisi Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea ajali hiyo akisema taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitatolewa baadae lakini taarifa zinasema Watoto 31 na Walimu wamefariki dunia.

 

 

Soma na hizi

1 thought on “Basi lenye Wanafunzi laua wanafunzi na walimu (karibu wote) Arusha (+ Picha)”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close